KAMISHNA BADRU AKAGA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UTALII ENEO LA NDUTU

October 10, 2025


Kamishna wa Uhifadhi wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru amefanya ziara katika eneo la Ndutu lililopo hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kukagua ukarabati wa Miundomninu ya utalii kuelekea msimu wa utalii katika eneo hilo ambalo ni maarufu kwa mazalia ya Nyumbu wanaohama.

Akiwa katika eneo hilo Kamishna Badru amekagua mradi wa ujenzi wa tenki la Maji lenye mnara wa mita 6 ambalo  likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita 50,000 za maji kwa ajili ya matumizi ya wageni wanaotembelea eneo hilo, maafisa na askari waliopo kanda ya Ndutu sambamba na hoteli na kambi za kulala wageni zilizopo Ndutu

Aidha, Kamishna Badru akiwa katika eneo hilo Kamishna Badru amesema Ngorongoro itaendelea kuboreshea mazingira ya uwanja wa ndege wa Ndutu ili kuwa rafiki kwa ndege zinazoleta wageni katika eneo hilo ambapo msimu wa kuzaa na kuhama kwa Nyumbu mwezi Desemba hadi Machi ndege ndogo 15 hadi 20 hutua kila siku katika eneo hilo kuleta wageni

Katika ziara hiyo Badru amezungumza na askari wa jeshi la uhifadhi katika kanda ya ndutu kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya ulinzi na uhifadhi katika eneo hilo ikiwemo kuimarsisha usalama wa wageni na mali zao pamoja na rasilimali za Wanyamapori na Misitu.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »