USHEREHESHAJI UTUMIE NIDHAMU,ITIFAKI, MAADILI, UBUNIFU NA UWAJIBIKAJI WA HALI YA JUU - WAZIRI MKUU

April 14, 2025

 Na. Vero Ignatius, Arusha


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana chama cha Kisima cha Mafanikio katika kuandaa miongozo, mafunzo ya kitaaluma, na mfumo wa urasimishaji wa washereheshaji nchini.

Ameyasema hiyo Jumapili (Aprili 13, 2025) katika Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania,(KCM) linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha,mbapo amesema kuwa fani ya ushereheshaji ni uchumi hivyo kwa kutambua umuhimu huo, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kaunzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao unakopesha hadi shilingi Milioni 100 kwa wasanii wakiwemo washereheshaji ili waweze kujiimarisha kimitaji na vitendea kazi,huku kuwa Serikali inatarajia kujenga Ukumbi wa Kimataifa ya Sanaa na Michezo ‘Arts and Sports Arena’ kwa shilingi bilioni 300.

“Aidha kupitia maboresho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 yaliyofanyika mwaka 2022, Serikali imeanzishwa tozo ya hakimiliki (copyright levy) ambapo asilimia 60 ya makusanyo inakuja kwenu moja kwa moja na asilimia nyingine 10 inakuja kwenu kupitia Mfuko”

Vile vile ameiagiza Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kwamba washereheshaji waliorasimishwa wanapewa nafasi za kushiriki katika matukio ya halmashauri, wilaya mikoa na maeneo mengine badala ya kuchukua watu wasiokua na weledi watakao iaibisha tasnia na kupunguza hadhi ya shughuli.

"Hawa wote wanatoka kwenye halmashauri zetu sasa mbapataje shida kupata mshehereshaji wakati kila kitu kipo hapo halmashauri mbakosaje mtu wa kuandaa matukio yenyenweledi yenye kuangalia Itifaki ya kiongozi gani magombana wakuu wa idara hii siyo kazi yenu ni taaluma ya watu. Alisema

Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia VETA na BASATA kuangalia kozi maalum kwaajili ya mafunzo ya Ushereheshaji na upangaji matukio ili vijana wapate stadi za ki taaluma na vyeti vinavyotambulika rasmi.

Awali akitoa salam kwa ya Mhe. Waziri Mkuu katika Kongamano la Wafawidhi wa Matukio Kisima cha Mafanikio(KCM )Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Palamagamba Kabudi alitoa rai kwa washerehesgaji kuangalia namna bora ya kutumia mitandao ya kijamii kama eneo la kuelimisha na siyo kudhalilisha au kupotosha jamii huku akiwataka kuendelea kulinda tunu za Taifa kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania katika kila jukwaa

Aidha amesema tasnia hiyo ya wafawidhi wa matukio ni kazi inayohitaji umakini mkubwa,maadili nidhamu,kujitambua, elimu ubunifu na uwajibikaji wa hali ya juu ,vile vile ni sehemu kubwa ya kuingiza kipato na utambulisho wa taifa kuchochea maendeleo ya Taifa kupitia vipaji vyao

Mhe. Kabudi tuanajivunia kuwa na jukwaa la Kitaifa la kuwaendeleza washereheshaji ,waelimishaji wahamasishaji,washauri na waandaaji wa matukio kupitia mafunzo ya kitaaluma na majukwaa ya mijadala mbalimbali na kuiweka taaluma hiyo katika ramani ya maendeleo ya kijamii na nchi

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Ester Kimweri amesema kuwa chama hichokimejengwa kwenye dhamira ya kusaidia ukuaji wa stadi za kuzungumza na kuwasilisha ili kujenga ueledi katika ushereheshaji kwenye shughuli za kijamii kiutamaduni hafla za kiserikali ,sekta binafsi shughuli za kisiasa na uratibu wa matukio yenye tija kwa Taifa

Kimweri amesema wao kama wadau wa sekta hiyo wanaonesha nia yao ya dhati kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa vitendo kwa kuuelimisha, kuuhamasisha, kuburudisha na kufundisha sambamba na kuendelea kuheshimu sheria, kulinda rasilimali, mali za umma, kushiriki shughuli za maendeleo ya jamii na kuhamasisha umma kuzijua kuzifuata sera ,miongozo, maelekezo ,mipango mikakati na vipaumbele vya Taifa, kupitia majukwaa yao wanapowasiliana moja kwa moja kwa wananchi kwenye shughuli na matukio wanayoyaratibu

Aidha Kisima cha mafanikio ni chama kilichosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2020 chini ya sheria ya Jumuiya ya 337 kwa usajili Na.SA 21669 ili kujishughulisha na nyanja za kitaaluma,kijamii kiuchumi na kitamaduni,vilevile kinatambuliwa na Wizara ya Habari ,Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa kwa Sheria Na.23 ya mwaka 1984 na kupewa kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa Nchini Na.BST-9684-190.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng