Na Anangisye Mwateba-Mkinga Tanga
Wizara ya Maliasili na Utalii ikishirikiana na idara zingine zinazojihusisha na utunzaji na uhifadhi wa Mazingira zimetakiwa kuhakikisha inatunza vyanzo vya Maji nchini katika maeneo yaliyohifadhiwa na Wakala wa Huduma za Misitu(TFS).
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Mkinga waliokusanyika katika viwanja Stendi ya mabasi kwenye kata ya Manza leo Februari 27,2025.
Mhe. Rais alisema kuwa ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Mto Zigi hadi Horohoro uendane na kutoa Maji kwenye vijiji unamopita ukianza na kuhudumia wananchi wa kijiji cha Mtimbwani huku ujenzi ukiendelea kutekelezwa kwenda maeneo mengine.
Vilevile Mhe. Rais aliitaka Wizara ya Madini Kufanya tathmini za kina kabla ya kutoa Leseni za Uchimbaji wa madini katika maeneo yaliyohifadhiwa ambayo yana vyanzo vya maji ili kuvilinda na kuzuia uharibifu wa mazingira ambao utaleta athari za kiafya kwa binadamu pindi watakapotumia maji hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula ambaye pia ni Mbunge wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga amemshukuru Rais Dkt. samia kwa Mradi Mkubwa wa Maji kutoka Mto Zigi kuelekea Horohoro ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 35.
![]() |
Mhe. Kitandula alisema kuwa uwepo wa Maji ya uhakika katika wilaya ya Mkinga ni ufunguo wa maendeleo ya kiuchumi kwa kuwa hapo mwanzo wawekezaji walikuwa wanakuja kuwekeza katika sekta ya viwanda na Utalii kwa ajili ya Hoteli walishindwa kwa kuwa hakukuwa na Maji ya uhakika.
Mhe. Kitandula pia hakusita kuzungumzia suala la wachimbaji wanaopewa vibali vya kuchimba madini kwenye maeneo yaliyohifadhiwa na Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) kutokupewa tena vibali hivyo kwa kuwa maeneo hayo Mengi ni vyanzo vya Maji , uchimbaji wa madini katika maeneo huhatarisha afya za binadamu ambao wanaenda kuyatumia Maji yanayotoka katika maeneo hayo
EmoticonEmoticon