TANI 22.5 ZA MAHINDI ZATOLEWA KWA KAYA 125 ZILIZOHMIA MSOMERA

December 21, 2024

Wananchi waliokubali  kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Tanga wameendelea kunufaika na upatikanaji wa mahindi yanayotolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Lengo la ugawaji wa mahindi hayo  ni kuwasaidia wananchi waliohamia kijijini hapo hivi karibuni kupata chakula kwa miezi 18 ijayo wakati wakiendelea  kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo. 

Kaya 125 zimegawiwa mahindi gunia mbili kwa kila kaya ambapo Kaya hizo zinajumuisha kaya 23 zilihamia Msomera tarehe 19 Desemba, 2024.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »