DKT BITEKO ASHIRIKI KUMUAGA DKT.NDUGULILE

December 02, 2024

 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 2, 2024 ameshiriki Misa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU).




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »