eGA YATOA MAFUNZO KWA KAMATI YA UONGOZI YA TEHAMA INEC

October 30, 2024

 


Na Mwandishi wetu, Dodoma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa TEHAMA wa taasisi hiyo.
 
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani, amesema kuwa Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika taasisi hiyo.
 
Amesema Tume inajitahidi kuwekeza katika TEHAMA, hasa kwa kutumia vifaa vya BVR (Biometric Voter Registration) katika uandikishaji wa wapiga kura, pamoja na mifumo ya kusimamia daftari, matokeo, wagombea, na waangalizi wa uchaguzi.
 
Aidha, Bw.Kailima amesema tayari Tume imepitisha miongozo saba ya kisera ili kuimarisha matumizi sahihi ya TEHAMA katika shughuli zake.
 
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 na sheria zinazohusiana na usimamizi wa teknolojia katika taasisi za umma.
 
Bw. Kailima ameitaja Miongozo iliyopitishwa kuwa ni pamoja na Sera ya TEHAMA, Mpango Mkakati wa TEHAMA, Mpango wa Kujikinga na Majanga ya TEHAMA, Sera ya Usalama wa TEHAMA, Mwongozo wa TEHAMA, Mwongozo wa Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA, na Mwongozo wa Uundaji wa Mifumo ya TEHAMA.

Nae Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Bw. Stanslaus Mwita amesema licha ya kuwa Tume ipo katika utekelezaji wa jukumu kubwa la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lakini wanatambua umuhimu wa mafunzo hayo.
 
Kwa sasa Tume inajukumuku kubwa la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lakini kwa kutambua umuhimu wa mafunzo haya na nasisi kama watumiaji wa kubwa wa mifumo ya TEHAMA  ili kuhakikisha kama taasisi inafuata sera na miongozo iliyowekwa, alisema Mwita.
 
Kiongozi wa Timu ya wakufunzi ambaye ni Meneja wa Usimamizi na Udhibiti na Viwango vya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Sultana Seif, amesema wanaendesha mafunzo kwa Kamati hiyo ya Uongozi wa TEHAMA ya Tume ili kuhakikisha wanaelewa na kuzingatia matakwa ya sheria ya serikali mtandao pamoja na viwango na miongozo.










Share this

Related Posts

Previous
Next Post »