CCM IMERIDHISHWA NA TAKWIMU ZA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAKAAZI LA WAPIGA KURA.

October 22, 2024


CCM iko tayari kupokea Matokeo yeyote ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa-.


Wingi huu wa Wananchi waliojiandikisha ni ishara tosha CCM itashinda kwa kishindo-.


Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam amezungumza hayo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, taarifa aliyoipokea kutoka kwa viongozi wa CCM wa mkoa huo leo, Jumanne Oktoba 22.2024


Nianze kuwapongeza Viongozi wa CCM kuanzia ngazi Mkoa mpaka Mabalozi pamoja na Wafuasi wa CCM na Wananchi kwa Ujumla yaani Mkoa mzima wa Dar es salam kwa kutoa Ushirikiano katika zoezi zima la Uandikishaji mpaka kufikia asilimia 96.7 hii ni faraja kwa CCM kwani Dar es salam ni uso wa Nchi.


Awamu hii Wananchi wamejiandikisha kwa wingi sana na hii imechagizwa na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hilo halina kificho kwa sababu miradi haitekelezwi hewani,Miradi ya Zahanati, Madarasa,Vituo vya Afya imetekelezwa kwenye Vijiji na Vitongoji hivyo Wananchi wameona kazi ya Dkt Samia Suluhu Hassan


CPA Makalla amesema endapo chama hicho tawala hapa nchini kitapoteza kwenye baadhi ya vitongoji, vijiji au mitaa vitaheshimu matokeo hayo na kwamba huo utakuwa wakati muafaka kwao kujitafakari na kujipanga kwa nini walipoteza eneo hilo, ili uwe njia ya kufanya vizuri kwenye uchaguzi ujao


amesema taarifa iliyotangazwa na Waziri wa Tamisemi hakushangaa kwani takwimu ndani ya Chama zinaonyesha kumekuwa na muitikio mkubwa ni kwa sababu ya kukubalika kwa CCM hasa utekelezaji wa Ilani mzuri ya Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi hilo halina kificho na Watanzania wanaona .



"Miradi hii haitekelezwi hewani, miradi hii ya Zahanati, madarasa, vituo vya afya inatekelezwa katika maeneo ya vitongoji, vijiji na mitaa kwa hiyo wananchi wa Tanzania wanaona hivi vitu, wanaona namna ambavyo Rais Samia (Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa) amevunja rekodi ya kupeleka fedha za maendeleo katika kila eneo, na kwa maana hiyo wamevutiwa sasa kuona wanaweza wakawasimamia viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaopelekewa fedha hizo ili kuona maendeleo yanaendelea kuwepo kwenye vijiji na mitaa yao ndio maana kuwekuwa na muamko huu" -Makalla


Akizungumzia kuhusu hamasa ya Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Daftari la Mpiga kura- amesema


Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Taifa na Rais Dkt Samia amekuwa chachu kubwa kwa Wananchi wengi Kujiandikisha kwenye daftari la Mkazi kwa sababu Wananchi wengi walipata ishara kuwa Uchaguzi ni muhimu kwani wengi waliona kama Rais amejitokeza na huyu ndie anaepeleka pesa mpaka ngazi ya kijiji wengi wakajitokeza amekuwa Kiongozi wa mfano lakini upande wa pili hawakufanya hivyo.


CCM Dkt Samia amejiandikisha ,Balozi Nchimbi amejiandikisha,Wa NEC , Viongozi wote wa Jumuiya na Mikoa mpaka Wilaya wamejiandikisha


"Wananchi walipomuona Dkt Samia anaenda Kujiandikisha pamoja Viongozi wakuu wa Chama na Serikali kuanzia ngazi za Mikoa mpaka Wilaya kila eneo hilo tu lilitosha kuleta hamasa kwamba Uchaguzi huu ni muhimu na mana wakajitokeza" CPA Makalla




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »