Benki ya CRDB yazindua mashindano ya CRDB Bank Supa Cup 2024

September 03, 2024

Benki ya CRDB imezindua rasmi msimu mpya wa mashindano ya mpira wa miguu na mpira wa pete yanayowahusisha wafanyakazi wake yanayotambulika kama “CRDB Bank Supa Cup 2024”, yaliyoanza kutimua vumbi siku ya Jumapili, tarehe 1 Septemba 2024, Jijini Dodoma.

Mashindano hayo yanayolenga kuongeza ari, nguvu na ushirikiano baina ya wafanyakazi wa benki hiyo, yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya John Merlin. 
Akizungumza wakati akifungua mashindano hayo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, alisema kuwa, “Baada ya kusambaza tabasamu kwa wananchi wa Tanzania na kuvuka mipaka ya nchi kwenda nchini DR Kongo na Burundi, sasa ni zamu ya tabasamu hilo kurudi nyumbani tena na sasa ni kwa wafanyakazi.” 

Michuano hiyo  inahusisha wafanyakazi wa Benki ya CRDB kutoka matawi mbalimbali, pamoja na makao makuu wakishindana vilivyo kuwania kombe la msimu.
Aidha, mashindano hayo yalienda sambasamba na programu ya kujitolea kwa wafanyakazi wa benki hiyo, ambapo siku ya Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2024, wakiongizwa na Mkurugeni wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa walitoa misaada ya vifaa vya kazi katika hospitali ya rufaa ya Dodoma, kuchangia damu, pamoja na kutoa chakula na vinywaji kwa wagonjwa wa hospitali hiyo.

Benki ya CRDB ilianzia programu hiyo maalumu ya wafanyakazi wake kujitolea ikilenga kusogea karibu kwa jamii wanayoihudumia. 
Akizungumza, Rutasingwa alisema, “Sisi kama Benki ya CRDB ni sehemu ya jamii na hatuna budi kurudi kwao kuchangia chochote kile ili kusogeza mbele maendeleo yetu. 
 
Programu hii ilizinduliwa visiwani Zanzibar mwezi uliopita na tunatarajia kuendelea kufanya hivyo katika mikoa mingine baada ya hapa Dodoma.”







Share this

Related Posts

Previous
Next Post »