WATAALAMU WA KUPAMBANA NA UJANGILI WAKUTANA ARUSHA

October 10, 2023
Na Mwandishi Wetu-Arusha

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) amesema ili kupambana na uhalifu wa wanyamapori kunahitaji ushirikiano, kuchangia rasilimali fedha na kupashana habari pamojag na kuwa na operesheni za pamoja kikanda

Hayo ameyasema wakati akifungua mafunzo kwa Wahifadhi Wanyamapori kutoka katika nchi za Afrika na Asia ambao wamekutana Jijini Arusha kwa lengo la kupeana uzoefu juu ya mbinu mpya na bora za kupambana na changamoto ya ujangili na usafirishaji haramu wa Nyara zitokanazo na wanyamapori na misitu.



Mhe. Kitandula aliongeza kuwa wahifadhi wanyamapori wanatakiwa kutambua kuwa utekelezaji wa sheria za wanyamapori kwa ushirikiano ni muhimu na ni moja ya mahitaji muhimu ya kupambana na ujangili kwa ufanisi na kuongeza utaalam katika kudhibiti uhalifu kwenye maeneo ya wanyamapori.

Vilevile, Mhe. Kitandula alifafanua kuwa mafunzo hayo yanawapa washiriki nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu, kukuza ujuzi na maarifa yanayohitajika katika kujenga mtandao wa ufanisi kwa utekelezaji wa sheria za wanyamapori na udhibiti wa vitendo vya ujangili wa Wanyamapori na Misitu.

“Kutokana na viwango vya sasa vya uhalifu wa wanyamapori katika Bara, na bidhaa haramu hasa pembe za tembo, pembe za kifaru, na magamba ya pangolin kusafirishwa nje ya nchi katika siku za hivi karibuni, kuna haja ya kuimarisha uwezo na kukuza ushirikiano kati ya vyombo vya utekelezaji wa sheria kupitia kuongeza ufuatiliaji na kushirikishina habari ” aliongeza Mhe. Kitandula

Naye Mkurugenzi wa mkataba wa LATF(LUSAKA AGREEMENT TASK FORCE) Edward Phiri alisema kwamba mafunzo hayo yanaonyesha ushirikiano uliopo katika kukabiliana changamoto ya usafirishaji wa nyara zitokanazo na wanyamapori pamoja na misitu.



Aidha, aliongeza kuwa wataalamu hao wanaenda kupata mafunzo ya kinadharia na vitendo yanayoendana na mazingira ya sasa kwa sababu wahalifu wameongeza ubunifu hivyo ni bora wataalam hao wakapata mbinu mpya za kukabiliana na ujangili wa wanyamapori na misitu.

Mafunzo hayo yanajumuisha wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali zinahusika na uhifadhi wa wanyamapori na mazao ya misitu Barani Afrika na Asia.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »