MAAFISA UHAMIAJI NGAZI YA KATA WATASAIDIA KUPUNGUZA WIMBI LA UINGIAJI WAHAMIAJI HARAMU MKOANI TANGA

April 30, 2018
UWEPO wa Maafisa Uhamiaji Ngazi ya Kata umetajwa kuwa mwarobaini wakuzibiti kwa kiasi kikubwa kwa kupunguza wimbi la uingiaji wa wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia mkoani Tanga kutokana na kuwepo kwa ushirikiana baina yao na wananchi wa maeneo husika.

Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga (DCI) Salum Farahan Pichani Juu wakati akizungumza na mtandano huo ambapo alisema kwani maafisa hao wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na wananchi .

Alisema hatua hiyo itakuwa suluhisho la kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya wahamiaji hao kuingia mkoani hapa kwani itawasaidia kuweza kuwabaini kutokana na kuwepo kwa maafisa hao kwenye ngazi hizo.

“Labda niseme tu mipango ya kuhakikisha tunakabiliana kwa vitendo wimbi la wahamiaji haramu nchini tumeanza mikakati yake kwa kuimarisha kwenye kata na sasa tuna Afisa Uhamiaji kwenye kila kata nah iiitasaidia kuweza kushirikiana na wananchi kuzuia vitendo vya uingiajiwao “Alisema.

Alisema maafisa uhamiaji hao wanafanya kazi zaidi kwani wakati mwengine wanalazimika kwenda kwa wananchi hususani vijijini ambapo wahamiaji wamekuwa wakitumia njia za mipakani.

Hata hivyo alisema hivi sasa pia wameweka vizuizi kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga kwa lengo la kuzibiti uingiaji wao ambavyo ni eneo la Vijinga, Horohoro wilayani Mkinga, Mkata wilayani Handeni na Kilapura wilaya ya Tanga.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »