Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta
utepe pamoja na viongozi wengine kuashiria ufunguzi wa kiwanda kikubwa cha Kusindika na kuzalisha
mafuta ya Alizeti cha Mount Meru Millers kilichopo mkoani Singida. Kiwanda
hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu tisini za mafuta ya alizeti kwa mwaka.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda hicho kikubwa cha kusindika Alizeti cha
Mount meru millers kilichopo mkoani Singida. Wengine katika picha ni Mkuu wa
mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu
Nchemba, mmiliki wa Kiwanda hicho Atul Mittal mwenye nguo nyeupe na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles
Mwijage.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika Alizeti cha
Mount Meru Millers kilichopo mkoani Singida.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akielekea kwenda kukagua shughuli mbalimbali za kiwanda hicho cha usindikaji wa
Alizeti kilichopo mkoani Singida.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda
hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliohudhuria hafla
ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa Alizeti.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifurahia jambo na Waziri wa Mambo ya
Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa kiwanda hicho
kikubwa cha Usindikaji wa Alizeti mkoani Singida.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Mount Meru Millers Atul Mittal mara baada ya
kumaliza kutoa hotuba yake ya uzinduzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa
Alizeti mkoani Singida. PICHA NA IKULU