Waziri wa Habari,Sanaa,Utamduni na Michezo Dkt Harson Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaofanyika kwa siku tano jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama
cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas akizungumza katika mkutano hu unaofanyika katika Ukumbi wa mikuano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) ,Pascal Shelutete akitoa taarifa ya TAGCO kwa washiriki wa Mkutano huo .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ,Hudson Kamoga akifuatilia hotuba zilizotolewa wakati wa mkutano huo.
Katika Mkutano huo pia kumetolewa Vyeti kwa Wadau walioshiriki katika kufanikisha mkutano huo .
Mmoja wa Wadau waliosaidia katika kufanikisha mkutano huo akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Dkt Harson Mwakyembe.
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Dkt Harson Mwakyembe ,Waziri wa Habari,Sanaa ,Utamaduni na Michezo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
WAZIRI wa Habari,Utamaduni ,Sanaa
na Michezo ,Dkt Harson Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza
majukumu yao kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na Taratibu za serikali huku akiwataka
kuzingatia malengo ya kitaifa waliyojiwekea katika kikao kilichopita.
Mbali na agizo
hilo Dkt Mwakyembe pia amesema serikali haita wavumilia maafisa habari ambao hawatambui wajibu wao huku akiwafananisha na maafisa habari hewa
ambao wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari
mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.
Dkt Mwakyembe ameyasema hay oleo wakati akifungua kikao
kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikali ,kinachofanyika katika
Ukumbi wa mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha kinachowakutanisha zaidi
ya Maafisa Habari zaidi ya 300 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji
wa majukumu yao.
Katika kikao hicho kinachoenda
sambamba na Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini
(TAGCO)kinafanyika wakati kukiwa bado kuna changamoto katika kada ya maafisa
Habari wa taasisi za Umma ikiwemo uharaka wa ufikishaji wa taarifa za serikali
kwa umma .
Katika mkutano huo Mkurugenzi
Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas amewakumbusha
washiriki wa mkutano huo kuenenda kimkakati huku akitoa nukuu za mcheza filamu
Mashuhuri nchini Marekani ,Anord Schwazniger .
Naye Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa ,Tanzania ,Alvaro Rodriguez amesema serikali ina umuhimu mkubwa wa
kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazo
iunganisha Dunia .
“Umoja wa Mataifa unaiona
Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana,Demkorasia ,kufikia uchumi
wa kati ,Elimu Bure,kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa
ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi.”alisema
Rodriguez.
Katika mkutano huo TAGCO ambacho
ni chama kisicho cha kiserikali (NGO) kikiwa na madhumuni ya kukuza Mawasiliano
na kuongeza Usambazaji wa Taarifa ndani
ya serikali na kati ya serikali na Wananchi kimekabidh vyeti kwa Wadhamini wa mkutano huo
ikiwemo Kampuni ya Clouds Media Group.
Mwisho .