Watu
wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) mkoani Tanga wametakiwa kuachana
na kasumba za kukimbia kwa waganga wa kienyeji na kuendelea na
utaratibu walipangiwa na wahudumu wa afya
wa kutumia dawa kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia matatizo
makubwa.
Hayo
yalisemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt Asha Mahita wakati
akifungua warsha ya kuwajengea uwezo Waviu washauri ili waweze
kuunganisha jamii kwenda katika vituo vya afya.
Warsha hiyo inaratibiwa na Shirika la AGPAHI mkoani hapa.
Alisema
vitendo vya wagonjwa kuacha dawa vinaweza kuwaweka kwenye wakati mgumu
ikiwemo kupata usugu ambao unaweza kupelekea kupoteza maisha kutokana na
kushindwa kufuata utaratibu
uliowekwa na kuwataka kuondokana na tabia za namna hiyo.
“Kuna
tabia ambayo imejengeka baadhi ya wagonjwa kuacha kutumia dawa na
kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kwani wanapoacha kutumia dozi na
kutumia dawa nyingine.. virusi vinakuwa
na usugu hali inayowasababishia hali mbaya zaidi na hata uwezekano wa
kupoteza maisha “Alisema.
“Mpaka
watu watambue kuwa hakuna dawa iliyothibitishwa kutibu VVU hivyo
waendelea kuzitumia dawa za kupunguza makali ya VUU (ARV) ikiwemo kuacha
kwenda kwa waganga wa kinyeji kwani
wanaweza kukumbana na matatizo makubwa sana “Alisema.
Aidha
alisema pia katika mpango wa mkoa wa Tanga wataendelea kuhamasisha
wananchi kwenda kwenye vituo vya afya ili waweze kujua afya zao ikiwemo
kuweza kuchukua hatua iwapo watabainika
wameathirika.
“Lakini
pia kwa watoto maana upimaji wao upo chini ikiwemo kuhakikisha watoto
wanaopata maambuzi wanaanzishiwa dawa mapema kwani zitawasaidia kuongeza
maisha yao na kuishi na afya
njema”Alisema.
Awali
akizungumza katika semina hiyo,Afisa Mradi Huduma Unganishi wa Jamii wa
Shirika la AGPAHI mkoani Geita Richard Kambarangwe alisema warsha hiyo
ni kuwapa elimu zaidi Waviu washauri
wanaosaidia kutoa huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC) kwa watu
wanaoishi na VVU.
Alisema
pia kuweza kuwasaidia kupata ujuzi zaidi ili kujifunza mbinu za
kuwatafuta na kuwaunganisha wateja wa CTC na vituo kwa jamii kuweza
kupunguza idadi ya kupotea kwa wateja.
“Lakini
pia takwimu za Tanzania na mkoa inaonyesha watu wengi wanaotumia dawa
za kupunguza makali ya VVU wanaweza kupotea kwenye huduma hivyo shirika
la AGPAHI mara kwa mara linazingatia
kutoa elimu itakayowasaidia watu kupata uelewa wa lishe na matumizi
sahihi ya dawa “Alisema.
Kaimu Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Tanga,Anita Temu akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Afisa Mradi wa Huduma Unganishi wa shirika la AGPAHI,Madina Paulo |
Afisa Mradi wa Huduma Unganishi wa shirika la AGPAHI,Madina Paulo akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga |
Afisa Mradi Huduma Unganishi wa Jamii wa Shirika la AGPAHI mkoani Geita Richard Kambarangwe akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye semina hiyo |
Afisa Mradi Huduma Unganishi wa Jamii wa Shirika la AGPAHI mkoani Geita Richard Kambarangwe akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye semina hiyo |
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia |
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akijitambulisha kabla ya kuanza semina hiyo |
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakijitambulisha |
Mganga M kuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita katika akiteta jambo na Mratibu wa Ukimwi wa Jiji la Tanga,Moses Kisibo mara baada ya kufungua semina hiyo |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo mara baada ya kuifungua |