Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa koti la rangi ya
dhambarau na miwani akipata maelezo juu ya matumizi ya kamera za
barabarani kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa
Geita, Mkaguzi wa Polisi Mark Thomas Masawe wakati wa ukaguzi wa
mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
mkoani humu.
ofisa
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Hagai
Ruben akitoa maelezo kuhusu ukataji wa leseni za usafirishaji kwa Mkuu
wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama barabarani iliyofanyika kimkoa katika Mji Mdogo wa Katoro
Geita.
Wataalam
wa Jeshi la Zima Moto na Wokozi Mkoa wa Geita wakiwaeleza wajumbe wa
Baraza la Usalama barabarani la Mkoa wa Geita juu ya matumizi
mbalimbali ya mitungi yenye Gesi ya kuzima moto wakati wajumbe hao
walipotembelea banda la kikosi hicho.
Emmanuel
Chacha mtaalam kutoka Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Geita (GGML)
akitoa maelezo kuhusu matumizi ya vifaa vya wokozi katika maeneo ya
migodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na wajumbe wa baraza la Usalama
barabarani .
Wanafunzi
wa Shule za Msingi za Mji wa mdogo wa Katoro wakiwa katika maandamano
ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani yakipita mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha).
Waendesha
Piki Piki maarufu kama boda boda wakiwa katika maandamano ya
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika Katoro
Geita.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akimpongeza Alfred Hussein Mkuu wa
Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Geita wakati wa maadhimisho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel akihutubia wananchi(awapo katika Picha)
wakati wa wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama
barabarani Mkoani Geita.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo akizungumza na wanahabari
baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani
Mkoani Geita.
(PICHA ZOTE NA BALTAZAR MASHAKA)