Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiangalia
chanzo cha maji katika milima ya Urugulu, Mjini Morogoro, akiwa katika ziara ya
mkikazi Mkoani Morogoro Mpina alielezwa kuwa chanzo hico cha maji kinaharibiwa
na shughuli za binadamu.
Kulia
Mratibu wa Mazingira kanda ya mashariki kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Jafari Chimgege akiongea jambo wakati wa
Oparesheni ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha Sukari Mtibwa.
Katikati
Naibu Waziri Mpina akisukuma toroli baada ya kumaliza zoezi la usafi wa
mazingira wilayani Mvomero, kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Mohammed Mussa
Utali.
Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Mohammed Mussa Utali akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri Mpina kabla ya kuanza zoezi la usafi wilayani humo.
NA EVELYN MKOKOI - MVOMERO
Akiwa katika ziara ya
ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
ametoa maagizo kwa kiwanda cha Mtibwa sukari kuieleza serikali kwa nini bado
kiwanda hicho kinaendelea kutumia magogo katika uzalishaji wake licha ya maelekezo
aliyowahi kuyatoa kiwanda hapo katika ziara yake mwaka mmoja iliyopita
iliyowataka kutumia mfumo rafiki kwa mazingira.
Alipokuwa ziarani kiwandani hapo
mwaka Jana. Mpina aliagiza kiwanda hicho kutoka katika mfumo wa uzalishaji kwa
kutumia njia hiyo ya magogo ambayo si rafiki kwa mazingira ambapo kiwanda
kilipewa muda wa mwaka mmoja kubadilisha mfumo huo sambamba na mfumo wa
utiririshaji wa majitaka toka kiwandani hapo jambo ambalo wamelitekeleza kwa
kujenga mfumo wa kisasa wa uondoshwaji wa maji taka,hatua ambayo imempelekea
Naibu Waziri Mpina kukipongeza kiwanda hicho.
Kwa Upande Wake Meneja uzalishaji
wa kiwanda hicho Bw. Abel Magese alimueleza Mpina kuwa kiwanda hicho kipo
katika hatua ya kujenga mabwawa makubwa ya kisasa ya kutunzia maji ya uzalishaji.
Kufuatia taarifa hiyo,Mpina aliwataka waandike barua Kwa mamlaka husika yaani NEMC kupitia
Serikali ya Mkoa na bonde la Wami Ruvu ili kuweza kufanyika Kwa tathmini kwa
athari ya mazingira na kuwezesha mchakato huo kwenda kwa haraka.
Mpina pia alikipongeza kiwanda
hicho kwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa sukari kutoka Tani 15,000 kwa mwaka
jana. mpaka tani 30,000 za sukari kwa mwaka huu, na kusema kuwa ongezeko hilo
litachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa sukari nchini
Aidha, Mpina pia
alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa
kuajiri wahitimu kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini pamoja na kuwachukua
wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo.
Wakati huo huo, Naibu waziri
Mpina Alitembelea vyanzo vya maji vya milima ya Urugulu na Ruaha mpakani mwa
wilaya ya Mvomero na Kilosa akiwa na lengo la kujionea utunzanji wa vyanzo
hivyo vya maji na misitu ya hifadhi inavyotekelezeka.
Mpina amemaliza Ziara yake ya
siku mbili Mkoani Morogoro leo.
EmoticonEmoticon