Karakana za kisasa zilizojengwa katika Dampo la jiji la Mwanza.
Mwenye Kofia Nyeupe Msimamizi wa
Dampo la jiji la Mwanza (Site Manager) Bw. Desderius Pole akimuonyesha
Naibu Waziri Mpina tokea mbali karakana za kisasa hazipo katika picha
zilizojengwa katika Dampo la jiji hilo, kulia ni wana habari kazini.
Afisa Mazingira wa jiji la Mwanza
wa pili kulia Bi Lidya Nyeme, akimuelezea Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira na Ujumbe wake katika picha kuhusu
machinjio ya kisasa ya Jiji la Mwanza iliyojengwa kwa ufadhili wa Bank
ya Dunia kupitia Mradi wa hifadhi ya mazingira ya Ziwa Victoria (LVEMP)
uliyopo chini ya Wizara ya Maji, Naibu Waziri Mpina yupo katika Ziara
ya kikazi jijini Mwanza.
…………………………………………………..
NA EVELYN MKOKOI – MWANZA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu w
rais Muungano na mazingira amelipongeza jiji la mwanza kwa hatua
iliyochukua ya kutunza mazingira kwa ujenzi wa Dampo na machinjio ya
kisasa kwa lengo la kupunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira
kutokana na utupaji taka ovyo.
Aidha, amelipongeza jiji hilo kwa
maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya dampo la kisasa kama mizani ya
kupimia taka, ofisi na maabara ya kemikali katika dampo hilo uliopelekea
jiji hilo kufuzu kupata ufadhili kupitia Bank ya dunia licha ya kutumia
mapato ya ndani.”Nikiangalia naona mmewekeza kama zaidi ya milioni 700
ambayo mumewekeza kama manispaa ya Jiji la mwanza.” Alisema Mpina.
Mpina aliongeza kwa kusema kuwa
kwa jiji la mwanza kufanya hivyo ni hatua kubwa na kulitaka jiji hilo
kuendelea na ari hiyo katika suala zima la hifadhi na utunzaji wa
mazingira. Mpina pia aliitaka Manispaa hiyo kukamilisha kwa wakati hatua
nyingine za ujenzi wa dampo hilo kama vile za Tathmini ya Athari kwa
Mazingira na kulipa fidia kwa wananchi na kaya zilizobakia ili
kukamilisha upanuzia wa dampo hilo, na kuepuka vipingamizi visivyo vya
lazima.
Katika hatua nyingine Mpina pia
aliwapongeza wahisani kwa kuiamini serikali ya awamu ya tano katika
mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika suala zima la hifadhi
ya mazingira. “Naamini katika mradi huu unaokuja wa zaidi ya shilingi
Bilioni 19.8 miundombinu ya hapa itakuwa ni mizuri na rafiki zaidi kwa
mazingira, kikubwa zaidi ni kuwekeza nguvu zetu katika mradi huu na
kuhakikisha kuwa unatekelezwa kama ulivyopangwa”. Alisema Mpina.
Wakati huo huo Naibu Waziri Mpina
alitembelea Machinjio ya kisasa ya jiji la Mwanza na kujionea ukarabati
wa machinjio unahusisha utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka katika machinjio hayo
ambapo mtambo huo utazalisha pia biagas kwa ajili ya kuzalisha
nishati ya umeme na kuzalisha mbolea. Ukarabati huo unahusisha pia
ujenzi wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia nyama kitakachowezesha
wafanyabiashara ya nyama kusafirisha nje ya nchi.
Katika hali isiyo ya
kawaida Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha
Senrun Investment kilichopo eneo la Igoma na kusisitiza kiwanda hicho
kiendelee kufungwa kutokana na kubainika kuendesha shughuli zake kinyume
na Sheria kwa kutokuwa na vibali vya uchenjuaji dhahabu, cheti cha
Tathmini ya athari kwa Mazingira na kibali cha matumizi ya kemikali
kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. “Nasisitiza kwamba kiwanda hiki
kiendelee kufungwa kama ambavyo NEMC wamekifunga na nawataka wamiliki
kuwasilisha vibali husika ndani ya siku 7 na wasiendelee na uzalishaji
mpaka watakapomaliza zoezi la kufanya tathmini ya athari kwa mazingira”.
Awali kiwanda hicho kilifungwa na NEMC kufuatia malalamiko ya wananchi
wa maeneo hayo kwa kutiririsha maji yenye kemikali, kutoa moshi mkali
kutokana na uchomaji wa taka zenye sumu na kutokuwa na vibali muhimu vya
kuruhusu uendeshaji wa shughuli za uchenjuaji dhahabu.
EmoticonEmoticon