Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Mungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina ambaye pia ni Mbunge wa
Kisesa akiongea na wadau hawapo katika picha kuhusu utekelezaji wa mradi
wa chanzo cha maji cha Igombe, Mwandoya Mkoani Simiyu.
Chanzo cha maji cha ajabu kikiwa
chini ya Mchanga, ambapo juu hakuna maji yoyote yanayoonekana badala
yake ni mchanga unaonekana kama mto uliyokauka maji, chanzo hiki
kipokatika kijiji cha Igombe wilayani Meatu.
Jengo linaloonekana katika Picha
ni sehemu ya kupokelea maji yanayotoka chini ya mchanga na kupanda bila
pump katika mabomba ndani ya jengo hilo na kuja kusambazwa kwa wakazi
kwa vijiji jirani kwa matumizi ya nyumbani
Jengo linaloonekana katika Picha
ni sehemu ya kupokelea maji yanayotoka chini ya mchanga na kupanda bila
pump katika mabomba ndani ya jengo hilo na kuja kusambazwa kwa wakazi
kwa vijiji jirani kwa matumizi ya nyumbani
………………….
NA EVELYN MKOKOI – IGOBE
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameagiza chanzo cha maji
cha kipekee ambacho kinatoa maji chini ya Mchanga, kilichopo katika
kijiji cha Igobe Wilayani Meatu kukamilika ifikapo mwisho wa Mwezi huu
ili kusaidia utoaji na usambazaji wa huduma ya maji safi na salama
katika vijiji jirani na chanzo hicho na kata ya Mwandoya kwa ujumla.
Akiendelea na ziara ya kikazi
Jimboni Kisesa, Mpina ameelezwa kuwa ucheleweshwaji wa kukamilika kwa
matumizi ya chanzo hicho cha maji yametokana na kucheleweshwa kwa malipo
kwa mkandarasi Mbesso Constraction Company ltd. ambapo kati ya
fedha za mradi shilingi milioni 502, zinazotelewa na serikali kupitia
Wizara ya maji na umwagiliaji ni kiasi cha fedha cha shilingi milioni
114 tu ndizo zilitoka na kutumika mpaka sasa.
Mpina, ameagiza kufanyiwa kazi kwa
kasoro zilizojitokeza katika mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia
takribani watu elfu nane katika kijiji cha Mwandoya na Igobe, ili
kumuwezesha mkandarasi kukamilisha kazi hiyo wa wakati.
“ Lazima Pawepo na usimamizi
madhubuti katika mradi huu ili wakazi wa maeneo jirani na mradi na mbali
na hapa waweze kunufaika na kama kutajitokeza kwa uzembe wowote
wahusika watawajibika kwa mamlaka.” Alisisitiza Mpina.
Katika ziara yake Naibu Waziri
Mpina pia alitembelea shule ya Sekondari ya Mwandoya ambapo aliongea na
walimu wa shule hiyo na kuwaeleza bila kuficha kuwa wamekuwa wakilaumiwa
sana kwa kuwa na mauhusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa shule hiyo na
kuwaasa kuacha tabia hiyo inayopelekea kuwaharibia maisha vijana hao na
kutoa wito kwa watu wazima katika kijiji cha Mwandoya kuachana kabisa na
tabia hiyo kwani ni kinyume na sheria na maadili ya Tanzania na kuwa
Serikali ya awamu ya tano ipo kazini.
Pamoja na hilo Mpina alisikiliza
changamoto zinazoikabili shule hiyo na kuhaidi kutatua baadhi ya
changamoto mpya, pia Mpina alikagua baadhi ya Mabweni mapya ya kisasa
yaliyojengwa katika shule hiyo.
Sambamba na hilo Naibu Waziri
Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa, alikagua ujenzi wa wodi Mpya ya
wazazi inayojengwa katika zahanati ya Mwandoya ambayo imefikia katika
hatua ya kupauliwa.
EmoticonEmoticon