Wachezaji
wa Taifa Stars wakipasha joto miili yao kabla ya kuanza mazoezi ya
nguvu kwenye Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria leo asubuhi
Juni 01, 2017. Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10,
2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019
zitakazofanyika Cameroon.
Makipa
wa Taifa Stars kutoka kushoto, Said Mohammed, Aishi Manula na Benno
Kakolanya wakivuta pumzi baada ya mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira
wa Miguu ‘Taifa Stars’ yaliyofanyika jana usiku kwenye Uwanja wa Tolip
Sports City jijini Alexandria jana usiku Mei 31, 2017. Taifa Stars
inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya
Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Daktari
wa Viungo wa Taifa Stars, Dk. Gilbert Kigadye akimfanyisha mazoezi ya
kifundo cha mguu beki wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama
Tshabalala katika mazoezi ya timu ya Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Taifa
Stars’ yaliyofanyika Uwanja wa Tolip Sports City jijini Alexandria jana
usiku Mei 31, 2017.
Wachezaji
wa Stars wakiwania mpira katika mazoezi ya nguvu yaliyofanyika leo.
Taifa Stars inajiandaa kushindana na Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la
Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
Wachezaji
wa Stars kutoka kushoto, Mohammed Hussein, Simon Msuva, Said Mohammed,
Ibrahim Ajib na Hassan Kessy wakionyesha faraja yao mara baada mazoezi
ya nguvu yaliyofanyika leo. Taifa Stars inajiandaa kushindana na
Lesotho Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania
tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za
mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.
EmoticonEmoticon