Judith Ferdinand, BMGHabari
Wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake, wanatarajia kupata burudani ya kukata na mundu kutoka kwa wasanii mbalimbali Kanda ya Ziwa katika tamasha la burudani "Nyanza Festival 2017".
Burudani hiyo ambayo itakua ya aina yake kwa kuwakutanisha wasanii kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, itafanyika Siku Kuu ya Pasaka kuanzia saa nne asubuhi mpaka majogoo kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mratibu wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, amesema mbali na burudani ya mziki pia kutakua na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Waandish wa habari za michezo Kanda ya Ziwa LASPOJA Fc na Bongo Movie, na Madjs na Watangazaji wa vipindi vya burudani watacheza na wafanyakazi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Naye Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi, amebainisha kwamba wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali siku hiyo.
"Zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu". Amesema Binagi.
Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.
EmoticonEmoticon