Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Chuo
kikuu cha shenyang kutoka nchini China kimeahidi kutoa ushirikiano na
Shirika la ndege la Air Tanzania kwa kutoa msaada wa kuwasomesha
wafanyakazi wa kampuni hiyo,ili waweze kumudu ushindani wa soko la
kimataifa.
Hayo
yamesemwa na mwalimu wa malezi wa chuo cha Shenyang, Shi Guangda katika
mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Global Education Link kwa wazazi
ambao watoto wao wanasoma urubani na Masuala ya anga katika chuo hicho.
“Tangu
Rais wetu wa China alipofika hapa tumekuwa na mahusiano makubwa na nchi
hizi mbili, hivyo kwa kuanza kama chuo chetu tutatoa ufadhili kwa
wafanyakazi wa shirika la ndege la Air Tanzania na kubadilishana mafunzo
katika chuo cha usafirishaji cha NIT na Shenyang” Amesema Guangda .
Kwa
upande wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Tanzania,Ladislaus
Matindi ameishukuru tasisi ya Global Education Link kwa kuwaunganisha
na chuo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa msaada mkubwa kwa kutoa mafunzo
kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Matindi
ametaja kuwa upatikanaji wa nafasi hiyo itasaidia kutoa motisha kwa
vijana wetu ambao wanafanya kazi katika shirika hilo na wengine ambao
wako nje kuwa na hamu ya kusoma masuala ya usafirishaji .
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Global Education link , AbduMalik Molell
alitumia fursa hiyo kuzungumza na wazazi hao juu ya swala la bima ya
wanafunzi amabo wanasoma chuo hicho katika swala zima la matibabu na
majanga mengine ambayo yatawakuta wanafunzi.
Mkurugenzi
wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akimkabidhi hati ya
ufadhili wa masomo Mkurugenzi wa shirika la ndege nchini Air
Tanzania,Ladislaus Matindi kwa ajili ya wafanyakazi wa shirika hilo
watakotakiwa kwenda kusoma China
Mkurugenzi
wa Shirika la Ndege la Air Tanzania Ladislaus Matindi akizungumza na
wazazi ambao watoto wao wanasoma masuala ya Anga nchini China
Mkurugenzi
wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akifafanua jambo kuhusu
masuala ya bima ya matibabu kwa wazazi ambao wamefika katika mkutano huo
Mlezi wa wanafunzi kutoka chuo Shenyang, akizungumza juu ya mazingira na ufadhili walio utoa nchini kwa shirika la ndege
Afisa
Biashara mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara upande wa Tantrade,
Stephene Kobelo akizungumza na wazazi juu ya namna watoto wanavyotakiwa
kuitangaza nchi
Baadhi ya Wazazi ambao wamefika katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini juu ya swala zima la bima ya matibabu kwa wanafunzi
Baadhi ya wakurugenzi wenza wa Tasisi ya Global Education Link wakisikiliza
Mmoja wa wazazi akichangia jambo juu ya kuboresha bima ya wanafunzi wanaosoma China
Wazazi na baadhi ya ndugu ambao watoto wao wanasoma nchini China wakifatilia mkutano.
EmoticonEmoticon