Kiongozi wa band ya East African Ngwasuma Original Band Kingombe Blaise wa pili kulia akiwa anafanya mambo katika ukumbi wa Filomena Bar uliopo Boma Ngo'mbe mkoani Kilimanjaro wakati wa onyesho lao walilofanya mwishoni mwa wiki hii
waimbaji na wanenguaji wa bendi ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanawapagawisha wakazi wa Bomang'ombe na mitaa yake
wanenguaji wa band ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanaonyesha viuno ikiwa wanacheza staili yao mpya ya Kampa Kampa tena
Rappa anaejulikana kwa jina la Papii katalogi akifanya yake ndani ya ukumbi wa Filomena Bar mkoani kilimanjaro
Habari picha na Woinde Shizza,Kilimanjaro
Bendi mpya iliongia mjini kwa kasi inayoongozwa na msanii maarufu Kingombe Blaise imewapagawisha wakati wa mji wa BomaNg'ombe na vitongoji vyake mara baada ya kutoa burudani kali ambayo iliacha historia
Bendi mpya iliongia mjini kwa kasi inayoongozwa na msanii maarufu Kingombe Blaise imewapagawisha wakati wa mji wa BomaNg'ombe na vitongoji vyake mara baada ya kutoa burudani kali ambayo iliacha historia
Wakiongea na blog hii baadhi ya washabiki wa mziki wa dance walisema kuwa wamefuarahi sana kupewa burudani na bendi hiyo , kwani walikuwa walikuwa na kiu ya mda mrefu kupata burudani kama hii
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Pendo Petro alisema kuwa bendi hii iko vizuri na imewapa burudani nzuri hivyo wanaiombea iendelee kudumu ili wao kama wananchi wa mkoa wa kilimanjaro waweze kuendelea kupata burudani
Akiongelea onyesho hilo kiongozi wa bendi hiyo Kingombe Blaise alisema kuwa wao wamejipanga kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa mkoa wa Arusha ,moshi naTanzania kwa ujumla
"sisi tumejipanga kuwapa burudani wapenzi wa mziki wa dance na kwa sasa tunafanya hizi show ila tunampango wa kuzindua Albamu yetu hivi karibuni na muda ukifika atutaacha kuwaaambia wapenzi wetu wa muziki huu ili nao waweze kutusapoti na tunawaaidi tutawapa burudani ya kweli ambayo kila mmoja ambaye anajua mziki wa dance ataifaurahia"alisema Kingblez
Aidha alisema kuwa pamoja kunaushindani mkubwa katika muziki huuu wao hawatetereki maana wanaamini kabisa amna bendi ambayo inawafikia kwa kutoa burudani hivyo wapenzi wa mziki wa dance waendelee kusubiri na waendelee kuwapa ushirikiano ili watimize malengo yao ya kuwapa burudani .
EmoticonEmoticon