Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi
wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks (katikati) wakati Balozi huyo
alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na
Uholanzi. Kulia ni Eugene Gies ambaye ni Katibu wa Uchumi na Sera za
Biashara wa Ubalozi huo nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya alipokuwa
anamfafanulia jambo Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim
Alsuwaidi (kulia) alipomtembelea Waziri Mwigulu ofisini kwake, jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano
kati ya nchi hizo mbili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza
Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks alipokuwa anamfafanulia jambo
Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, walipokuwa
wanajadiliana masuala mbalimbali ua ushirikiano kati ya Tanzania na
Uholanzi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba
Yahya. Kulia ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo
nchini, Eugene Gies. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto)akimsindikiza
Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi mara
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri
Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha
ofisini kwake Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks kwa ajili ya
kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
Uholanzi na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya
Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon