TUME
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshukuru Umoja wa Mataifa
kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa taasisi zisizo za kiserikali za
kujengea uwezo wa kuweza kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay wakati wajumbe
wa nchi za Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa programu za Umoja wa
Mataifa zinazotekelezwa nchini Tanzania walipozuru katika ofisi hizo kwa
mazungumzo.
“Kuna
ongezeko kubwa la ufahamu kuhusu haki za binadamu, upatikanaji wa haki
kwa makundi maalumu, uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na
kuboreshwa kwa huduma za kisheria na ukaribu wa serikali wa kufanyakazi
na wadau wa haki za binadamu,” alisema Massay akifafanua zaidi kuhusu
manufaa ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha haki za
binadamu nchini.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga (wa pili kushoto) akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe kutoka
nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa
Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Katibu
Mtendaji wa THBUB, Mary Massay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo
(kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Katika
mazungumzo yao na ujumbe wa nchi za Nordic ambazo ni Sweden, Denmark,
Norway Finland na Iceland kulikuwepo pia asasi mbalimbali zisizo za
kiserikali kama Women’s Legal Aid Center, Tanzania Women Lawyers
Association, Tanzania Women Judges Association, Legal Aid and Human
Rights Center, Human Rights Defenders Coalition, na Tanganyika Law
Society.
Katika
mazungumzo hayo asasi hizo zilielezea ufanyaji kazi wao mafanikio na
changamoto wanazokumbana nazo na umuhimu wa ufadhili wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa.
Akizungumzia
changamoto zinazokabili Umoja wa Mataifa, serikali na asasi Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema ipo haja ya kuwa na muono wa
muda mrefu wa kuratibu shughuli zinazohusiana na maendeleo endelevu.
Katibu
Mtendaji wa THBUB, Mary Massay akizungumzia shughuli mbalimbali
zinazofanywa na tume hiyo kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana
na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani)
ulipotembelea tume hiyo.
Alisema
kwamba mabadiliko ya kitabia kwa binadamu huchukua muda mrefu
kukubalika hivyo ni wajibu wa kila mmoja kufanya bidii ya kuhakikisha
kwamba maisha yanabadilika na watu wanakumbatia mambo ya kisasa
yanayochochea maendeleo yao na jamii
Akizungumza
kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic, Anders Rönquist,
ambaye ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la
Sweden (SIDA), alisema pamoja na changamoto zilizopo kitaasisi, kisiasa,
kifedha na kitamaduni maendeleo yaliyopo katika sheria na haki za
binadamu nchini Tanzania yanatia moyo sana.
Alisema
ipo haja ya serikali kuendelea kuhimiza mabadiliko na kwamba wao wapo
tayari kusaidia mkakati wa kuboresha masuala ya sheria na haki za
binadamu.
Kiongozi
wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA),
Anders Rönquist (kulia) akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi
hizo za Nordic ulipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Awa Dabo
(kulia), akizungumza katika mkutano huo ambapo alishukuru mataifa hayo
kwa kuendelea kusaidia programu za haki a binadamu nchini Tanzania.
Alisema kwamba haki za binadamu ni kitu cha msingi katika maendeleo kwa
kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila kuwapo na haki za binadamu. Alisema
kwamba maendeleo na haki za binadamu ni mambo yanayoshabihiana na
kuimarika kwake kunasaidia kuimarisha ustawi wa jamii. Alishukuru pia
serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamna masuala ya utawala bora na
haki za binadamu yamo katika mpango wa miaka mitano wa maendeleo ambao
unasaidiwa pia na UNDAP ll.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga akisisitiza jambo kwenye mkutano na wajumbe kutoka nchi za
Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC),
Theodosia Muhulo akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo
chake katika kuhakikishwa wanawake na watoto wapata msaada wa kisheria
wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na
wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mwansheria
kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Benedict Ishabakaki akizungumzia shughuli mbalimbali wanazofanya za
msaada wa kisheria wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura
aki-'share' uzoefu wake katika masuala ya sheria wakati wa ziara ya
wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika
ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa
Mwenyekiti wa THBUB wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura
akikabidhi zawadi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia)
baada ya kumalizika mkutano wa wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akikabidhi zawadi kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe.
Bahame Tom Nyanduga wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipokutana na uongozi wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Picha
juu na chini ni wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam
kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom
Nyanduga katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka nchi za Nordic
walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa
walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon