SERIKALI KUBORESHA MITAMBO YA KUCHAPISHA NYARAKA YA KIWANDA CHA UHAMIAJI KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM

November 15, 2016
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es Salaam.


Waziri Mwigulu akiwasili kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za makamishna wa Uhamiaji zinazojengwa Kijichi jijini Dar es Salaam kuzikagua.


Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Abbas Rovya (kushoto), akimpigia saluti Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mwigulu Nchemba (katikati) kabla ya kukagua nyumba hizo za kisasa. Kulia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI), Shaban Hamza.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia), akiangalia nyaraka mbalimbali zinazochapishwa katika kiwanda cha kuchapa nyaraka za Uhamiaji alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kijichi jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji (ASP), Singwa Mokiwa na Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Mwigulu mbali ya kutembelea kiwanda hicho na mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za makamishna wa Uhamiaji  pia alizungumza na wafanyakazi wa Uhamiaji makao makuu Kurasini. 
 Waziri Mwigulu akipata maelezo zaidi ya uchapishaji kwenye kiwanda hicho.
 Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Mwigulu.
 Waziri Mwigulu akiangalia nyaraka mbalimbali kwenye 
kiwanda hicho.
 Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Lusungu Ngairo (katikati), akimueleza jambo Waziri Mwigulu wakati wa ziara hiyo.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema itaboresha mitambo ya kuchapisha nyaraka ya Uhamiaji ili kupata nyaraka zenye ubora wa kisasa.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo mchana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati alipotembelea Kiwanda cha kuchapisha Nyaraka cha Uhamiaji kilichopo Kijichi Temeke jijini Dar es Salaam.

"Napenda kuwapongeza wenzetu wa Uhamiaji kwa kuwa na kiwanda cha kuchapisha nyaraka zao sisi kama serikali tutaongeza nguvu ndani ya taasisi hii ili kupata nyaraka bora zaidi " alisema Nchemba.

Mwigulu alisema nyaraka nyeti za serikali ni vizuri zichapwe na taasisi husika kama wanavyofanya uhamiaji jambo litakalosaidia kutozagaa hovyo mitaani.

Waziri Mwigulu aliongeza kuwa hivi sasa mpango wa serikali ni kutengeneza bidhaa zake kupitia taasisi zake kama ilivyo kwa viatu ambapo wameelekeza vitengenezwe na Magereza na kutumiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuzipa uwezo taasisi za serikali hasa majeshi kujiimarisha kwa kufanya kazi za viwanda zenyewe kama za utengenezaji wa madawati, uchapishaji wa nyaraka kama wanavyofanya Uhamiaji na nyingine nyingi.





Share this

Related Posts

Previous
Next Post »