Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA
wa soka Ligi Kuu ya Bara wamewasili jijni wakitokea Angola katika mechi
ya narudiano dhdi ya Espirance Sagdrada ya Angola.
Yanga
ambayo imefuzu hatua makundi wamewasili mida ya saa nane na dakika 45
na mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa kocha wa
timu hiyo Hans Van Pluijim amesema timu imefanya vizuri pamoja na figisu
figisu ambazo wamefanyiwa.
Amesema
anawapongeza viongozi wa Yanga kwa kupambana na hujuma lakini
wamefanikiwa kuingia hatua ya makundi na wamejifunza mengi Angola ambapo
watayafanyiwa kazi huku akiwapongeza wachezaji wake kwa juhudi
walizoonyesha uwanjani kuhakikisha wanafuzu.
"Wachezaji
wamefanya vizuri na wamejituma na kuhahakikisha wanavuka hatua hiyo na
wamejituma sana nawapongeza na tumejifunza mengi sana Angola,"amesema
Pluijm
Amesema
kikosi kwa sasa hakina cha kupoteza kitaendeea na kambi kuhakikisha
wanasonga mbele katika mashindano hayo lengo lao ni kuona wanafika hatua
ya fainali.
Golikipa wa timu ya Yanga Deogratius Munish Dida akizungumza na waandishi wa habari baada y kuwasili kutoka Angola.
Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga waliofika kuwalaki uwanja hapo mapema leo mchana.
Wachezaji wa Yanga wakitoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
Wachezaji wa Yanga wakitoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola
Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van De Pluijm akiwasabahi mashabiki wa timu ya Yanga
Wachezaji wa Yanga wakitoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Angola.Picha na Zaynab Nyamka,Globu ya Jamii.
EmoticonEmoticon