KIINGILIO TANZANIA v CHAD
5,000/= TU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kundi G siku ya Jumatatu
kati ya Tanzania dhidi ya Chad, bei ya chini ikiwa ni shilingi elfu tano
(5,000) tu.
Viingilio
vya mchezo huo vimegawanyika katika makundi matatu, ambapo kiingilio cha juu
kitakua shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa VIP A, na shilingi elfu
ishirini (20,000) kwa VIP B, na kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na orange
itakua shiligi elfu tano (5,000).
Tiketi
za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Jumapili saa 2 asubuhi katika vituo vinne
ambavyo ni kituo cha mafuta Buguruni (Buguruni), Ubungo Oilcom (Ubungo) na Dar
Live (Mbagala), na Jumatatu tiketi zitauzwa katika viunga vya uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Wakati
huo huo Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kubali kuwa mgeni rasmi
katika mchezo kati ya Tanzania v Chad utakaochezwa siku ya Jumatatu jijini Dar
es salaam.
TFF
pia inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa
kufanikisha ujio wa Waziri Mkuu kwa kufuatilia kwa karibu maombi ya TFF ya
tarehe 21/03/2016 ya kumuomba Waziri Mkuu awe mgeni rasmi katika mchezo huo.
Kwa
upande wa Taifa Stars iliyoweka kambi katika hoteli ya Urban Rose inaendelea na
mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa
marudiano dhidi ya Chad.
Waamuzi
wa mchezo huo kutoka nchini Djibouti wanatarajiwa kuwaisli leo jioni ambao ni
mwamuzi wa kati Djamel Aden Abdi, Abdilahi Mahamoud, Farhan Bogoreh Salim,
Farah Aden Ali, huku kamisaa wa mchezo akiwa Andrea Abdallah Dimbiti kutoka
nchini Sudani Kusini.
TFF YATUMA SALAMU ZA
RAMBIRAMBI KNVB
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limeomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Johann Cruffy
aliyefariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa Saratani.
Katika taarifa aliyoituma kwa Rais
wa Chama cha Soka cha Uholanzi, Rais wa TFF Jamal Malinzi amemwelezea Marehemu
Cruyff kama gwiji aliyetoa mchango mkubwa kama mchezaji na kocha katika timu ya
Taifa ya nchi yake na klabu za Barcelona, Ajax, Lavanet mwaka 1964 – 1977.
Tanzania tulikuwa na bahati ya
kutembelewa na Cruyff ikiwa ni sehemu ya kuitangaza klabu yake ya Barcelona na
kuendeleza mpira wa Vijana na maendeleo ya walimu wa soka nchini.
TFF inaungana nawe, familia ya
marehemu na wapenda soka ndani ya Uholanzi na duniani kote katika kuomboleza na
kusheherekea maisha ya Marehemu Johann Cruyff. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya
marehemu mahali pema peponi, Amen.
Johann Cruyff alizaliwa Uholanzi
tarehe 25 Aprili, 1947 na kuchezea klabu za Ajax, Feyenoord, Lavante, Los
Angeles, Washington Diplomats na timu ya Taifa ya Uholanzi kati ya mwaka 1966 -
1977 na baadae alizifundisha kalbu za Ajax, Barcelona na Catalonia.
--
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania
EmoticonEmoticon