Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akizungumza katika shughuli
ambapo Marekani iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa
kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika
Bandari ya Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kulia ni Kaimu Balozi wa
Marekani nchini, Virginia Blaser. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini,
Virginia Blaser akizungumza katika shughuli ambapo nchi yake iliikabidhi
Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na
Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo.
Kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe,wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Injinia Hamad Masauni, anayefuata ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akimuaga Kaimu Balozi wa
Marekani nchini, Virginia Blaser mara baada ya Marekani kuikabidhi
Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na
Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo.
Kushoto ni Ofisa Usalama Kanda, Ubalozi wa Marekani nchini, Bruce
Paluch. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akiwafafanulia jambo waandishi
wa habari mara baada ya Serikali ya Marekani kuikabidhi Tanzania Mbwa wa
Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio
lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (D/IGP), Abdulharam Kaniki. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akisindikizwa na Kaimu
Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto) pamoja na Maafisa
wengine wa ubalozi huo, mara baada ya kumaliza shughuli ya Marekani ya
kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya
Kulevya na Pembe za Ndovu katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es
Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon