Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi
kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu
na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kuhusu
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 ambao umepanda hadi
kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 kwa mwezi Septemba, 2015. Kulia
kwake ni Mtakwimu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Muhdin Mtindo. (PICHA NA
VERONICA KAZIMOTO)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam.
MFUMUKO wa bei
wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.3
kutoka asilimia 6.1 mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo amesema kuongezeka
kwa Mfumuko wa Bei kumesababishwa na kupanda kwa bei za bidhaa na
huduma zingine za kijamii ikiwemo chakula na nishati.
“Kupanda kwa
Mfumuko wa Bei wa mwezi Oktoba, 2015 kumechangiwa na ongezeko la bei za
vyakula kama vile Mchele ambao umeongezeka bei kwa asilimia 0.8, unga wa
muhogo umeongezeka hadi asilimia 0.7, nyama kwa asilimia 0.8, samaki
kwa asilimia 5.5, ndizi za kupika asilimia 0.7 na choroko kwa asilimia
0.9”, amesema Kwesigabo.
Bidhaa
zisizokuwa za vyakula kama vile vitambaa kwa ajili ya nguo za kike
zimepanda kwa asilimia 1.6, viatu vya kiume asilimia 1.1, mkaa asilimia
1.4 na gharama za kupata ushauri kwa daktari pia zimepanda hadi kufikia
asilimia 1.4.
Kwa upande
Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.1 ambao
ni ongezeko sawa na mwezi Septemba, 2015. Fahirisi za bei pia
zimeongezeka kutoka 159.04 hadi kufikia 159.17 kwa mwezi Oktoba, 2015.
“Fahirisi za
bei za vyakula vya nyumbani na migahawani iliongezeka kidogo hadi
kufikia asilimia 10.0 kutoka asilimia 9.4 kwa mwezi Septemba, 2015
ambapo bidhaa zisizokuwa za vyakula zimepungua kidogo kutoka asilimia
1.9 hadi asilimia 1.7 kwa mwezi Oktoba, 2015,” amefafanua Kwesigabo.
Kwesigabo
amesema kuwa Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa
mwezi Oktoba, 2015 umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 2.1 kutoka
asilimia 2.2 kwa mwezi Septemba, 2015.
EmoticonEmoticon