Michuano ya Kombe la Shirikisho ya (Azam Sports Federation Cup)
itafunguliwa rasmi kesho Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu
zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ambao jumla ya timu 64
zitashirki kuwania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho
barani Afrika mwaka 2017. Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara
na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD
ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani
Afrika mwaka 2017.
EmoticonEmoticon