Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Bw.Hamid M. Hamid (wapili kushoto) akisoma matokeo ya
wagombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu
Damian Lubuva.
Baadhi ya waandishi wa Habari wa
Ndani na Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya
wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu leo katika Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi
Chadema Bw. Matson Chizi akihojiwa na mwandishi wa habari wa Idhaa ya
Kiswahili, Sauti ya Ujerumani (DW) Bi.Hawa Bihoga kuhusu namna gani
analiona zoezi la utangazaji wa matokeo linafanyika.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wanne kushoto kwa waliyokaa
katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi
za Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika kutangazia matokeo ya
wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu leo jijini Dar es
Salaam.
Mwandishi wa habari kutoka Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela akimhoji mmoja wa
waangalizi wa uchaguzi ambaye ni Mwenyekiti wa SADC nchini Malawi
Bw.Justice Mbendera alipotembelea ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais
leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Anitha Jonas – MAELEZO.
EmoticonEmoticon