ACACIA YADHAMINI PAMBANO LA SOKA LA VIONGOZI WA DINI NA MABALOZI KUHAMASISHA AMANI

October 17, 2015

 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni
nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe
cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi
hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia,
anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo
 ………………………………………………………
NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na
kutwaa kombe.
Akitoa nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea
kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali
inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja
wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya
pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.
Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia  a ustawi wa kampuni,  Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake
imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo
Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii
katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua
viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi
ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika
kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona
tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa
hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani
safi wapenzi wa soka.
 Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya
mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia
kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa
kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili
kushoto)
 Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo
 Chikawe, akisalimiana na Alex Lugendo
 “Ball Boys” wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani
 Sheikh Alhadi akiwa kwenye mazoezi ya viungo na viongozi wenzake wa dini kabla ya mpambano huo
 Sheikh Alhadi akifumua shuti

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »