Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga,Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
PAMBANO la Mechi ya kirafiki kwa mahasimu wa soka mkoa wa
Tanga baina ya Coastal Union na African Sports limelazimika kusogezwa mbele
kutokana na siku lilatalochezwa kutakuwa na mechi kati ya timu ya Taifa ya
Tanzania “Taifa Stars” na Super Eagle ya Nigeria.
Viingilio kwenye mechi hiyo vitakuwa ni kati ya 5000 na 3000
kwa wakubwa na shilingi 1000 kwa watoto ili kuweza kutoa fursa kwa wapenzi wa
soka kushuhudia mechi hiyo.
Mchezo huo wa Stars na Super Eagle ya Nigeria utakuwa ni wa
kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazochezwa
mwaka 2017 nchini Gabon.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga,Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi
Mechi hiyo imeandaliwa pamoja na kudhaminiwa na Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii Mkoa wa Tanga (NSSF) ambapo kabla ya mchezo huo
kutakuwa na shughuli mbalimbali kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwemo
uandikishaji wa kujiunga na huduma za NSSF pamoja na kujiandikisha kwa mafao ya
matibabu yanayotolewa bure kwa wanachama wa mfuko pindi watimizapo miezi mitatu
ya uanachama hai.
Afisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga,Athumani Juma Mohamed akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari leo |
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Meneja wa shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Frank Maduga amesema kuwa sababu za kusogezwa
mbele mchezo huo ni kutoa fursa wapenzi wa soka nchini kuishuhudia timu ya
Taifa na baadae kujionea mechi hiyo siku itakayopangwa.
Alisema kuwa shirika hilo mkoani hapa limeamua kutumia siku
ya Jumamosi Septemba 5 mwaka huu kwa ajili ya kutoa elimu juu ya hifadhi ya
jamiio na huduma zinazotolewa na shirika hilo ikiwemo upimaji wa afya
bure,uandikishaji wa wanachama katika mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii na pia
kwa ajili ya mafao ya matibabu ili wanufaike na huduma hizo.
Afisa Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga,Chiku Mohamed Saidi akigawa taarifa kwa waandishi wa habari kwenye mkutano huo.
Aidha alisema kuwa wameandaa michuano ya mpira wa miguu kwa
wanawake itakayofanyika siku hiyo ikihusisha timu za Pangani, Muheza na timu
mbili za wilaya ya Tanga ambapo mshindi wa mashindano hayo atapokea zawadi za
ushindi pamoja na mshindi wa mechi ya watani wa jadi mjini Tanga iliyohamishiwa
Jumapili ili kutoa fursa kwa wadau wengine wa michezo kushuhudia na
kuishangilia timu ya Taifa inayocheza siku inayofuata.
Meneja huyo alisema kuwa siku ya Jumamosi kutakuwa na
burudani toka kwa vikundi vya sanaa na mechi za wanawake zitaanza saa 2:30
asubuhi hadi saa 6:00 na fainali kufanyika jioni.
Aliongeza kuwa pamoja na kusaidia timu za Tanga na kukuza
katika azma ya kukuza viwango vya soka mkoani hapa tukio linguine ni uzinduzi
wa huduma ya maji kupitia tanki lililojengwa upya katika kijiji cha Wazee Mikanjuni.
Afisa Mafao wa NSSF Mkoa wa Tanga na Mratibu wa Shughuli hiyo,Salum Maftaa kushoto akifurahia jambo na wadau wa michezo leo |
Alieleza kuwa pia wanachama hao wapya watapata fursa ya
kupata huduma ya matibabu ya ndani na nje ya mkoa zikiwemo hospitali za rufaa
ndani ya muda mfupi wa miezi mitatu bila kuathiri michango yao au kwa manene
mengine watapata matibabu ya bure.
Hata hivyo alisema kuwa huduma za mikopo inayotolewa na
shirika hilo kupitia vyama vya akiba vya kuweka na kukopa (Saccos) itapatikana
kwa wanachama wanaochangia si chini ya miwezi sita na ambao wamejiunga kwenye
Saccoss zinakidhi vigezo.
“Jamani ndugu zangu
kubwa kuliko yote,Uzee haukwepeki na pia ulemavu na umauti ni majanga ambayo
hakuna ajuaye yatamkuta lini na hivyo kinga ya uhakika dhidi ya kukosekana au kupungua
kwa kipato kwa mtu na wategemezi ni kujiunga na mpango wa hifadhi ya jamii
unaoendeshwa na NSSF “Alisema Maduga.