Mwigulu
Nchemba akiwasili eneo la Mkutano nje kidogo na Mji wa Babati hii leo
alipofika kwaajili ya Mkutano wa kampeni wa kuinadi Ilani ya Chama cha
Mapinduzi ya Mwaka 2015.Pia kuwanadi wagombea Udiwani na Ubunge kwa
Babati Mjini.
Kutoka
Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara Ndg.Ndekubali,Katikani ni
Mwigulu Nchemba na Mwisho kulia ni Mh.Chambili ambaye ni Mgombea Ubunge
Jimbo la Babati Mjini.
Mwigulu
Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Babati hii leo,Katika hotuba yake
amesisitiza Wananchi waachane na maigizo yanayofanywa na baadhi ya
wagombea Urais bali waamue moja la Kuchagua Rais Mchapa Kazi,.Mweigulu
amesisitiza Zaidi kuwa rekodi za wagombea Urais zipo wazi kila kona na
kwa rika zote.Hivyo watanzania watumie fursa hii kuhakikisha Taifa
linapata kiongozi Mchapa kazi ambaye ni J.Pombe Magufuli wa CCM.
Sehemu
ya mamia ya Wananchi waliofika kusikiliza Ilani ya chama cha Mapinduzi
wakishangilia namna Ilani ya chama hicho ilivyoweka bayana namna ya
Kutekekeleza shughuli za maendeleo katika Jimbo la Babati Mjini
Mh.Mwigulu
Nchemba akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini Ndg.chambili
wakiagana na Wananchi mara baada ya Mkutano huo wa kampeni wa CCM.
“CCM ni Ile Ile”
Picha na Sanga Jr.