MKUU WA MKOA MH.JOEL BENDERA AZINDUA MFUKO WA AFYA YA JAMII ULIYOBORESHWA ( CHF ) MKOANI MANYARA

August 23, 2015

New Picture
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkoani Manyara,Mkuu wa Mkoa Mh.Joel Bendera akiwasili katika viwanja vya Halmshauri ya Mji wa Mbulu akiongozana toka kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa –Bw.Ally Uledi,Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe.
New Picture (1)
Waziri katika ofisi ya Raisi Mauhusiano na Uratibu na Mbunge wa Hanang, Mary Nagu akawaelimisha wananchi umuhimu wa kujiunga na CHF ILIYOBORESHWA katika siku ya uzinduzi .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa shirika la Pharm Access kutoka Uholanzi Bw.Sicco Van Gelder ambao ndio wafadhili wa mradi huu wakishirikiana na NHIF.
New Picture (2)
Mkurugenzi wa CHF Bw.Eugene Mikongoti akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika moja ya banda la maonyesho ambapo wananchi walipata fursa ya kupimwa afya zao, kuchangia damu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zihusuzo CHF iliyoboreshwa na NHIF.Wengine toka kushoto ni Bw.Isaya Shekifu Kaimu Meneja wa NHIF – Manyara, Bw. Ally Uledi- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Dr.Heri Marwa Mkurugenzi wa Mradi wa Health Insurance – PharmAcess Tanzania
New Picture (3)
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akimkabidhi kadi ya CHF iliyoboreshwa mwanachama mpya aliyejiunga katika siku ya uzinduzi wa kimkoa wilayani Mbulu mkoani Manyara.
New Picture (4)
Mgeni rasmi wa siku ya uzinduzi wa CHF ILIYOBORESHWA mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Dr.Michael Kadeghe kukabidhi moja ya pikipiki tano zilizotolewa kwa maafisa wa CHF iliyoboreshwa ili kuwarahisishia kazi ya uandikishaji na uhamasishaji kwa wananchi wa tarafa tano za wilaya ya Mbulu.
New Picture (5)
Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Joel Bendera akiwasha moja ya pikipiki tano alizokabidhi kwa maafisa wanaoshughulika na CHF ILIYOBORESHWA mbele ya umati wa wananchi wa wilaya ya Mbulu katika siku ya uzinduzi wa mradi huu kimkoa.
……………………………………………………………………………
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Mh.Joel Bendera amezindua rasmi Mfuko wa Afya
ya Jamii Uliboreshwa (iCHF) mkoani Manyara.Uzinduzi huo uliohudhuriwa
na wageni mbalimbali akiwemo Mh.Mary Nagu(Mbunge-Hanang) na Waziri
katika ofisi ya Raisi Mahusiano na Uratibu, Wakuu wa wilaya za Hanang
na Mbulu pamoja Wawakilishi wa wizara ya afya na Ustawi wa Jamii,
ulifanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Mbulu.
Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kwa viongozi wa mkoa na wilaya kuhakikisha
kuwa wanasimamia vizuri mradi huu na kuhamasisha wananchi wajiunge kwa
wingi ili kufanikisha sera ya serikali ya kuboresha huduma za afya kwa
wananchi wote.
Pia halmshauri  za wilaya mkoani Manyara zimetakiwa kuweka bajeti maalum
itakayowezesha utekelezaji wa mpango endelevu wa kuziingiza kaya
maskini katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kila mwaka ili
kuwahakikishia huduma bora za matibabu.
Mradi huo wa iCHF mkoani Manyara unaendeshwa kwa ushirikiano baina
shirika la Pharm Access International (PIA) la Uholanzi, Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na Halmashauri za wilaya za Mbulu, Babati
na Hanang kwa lengo la kuboresha huduma na kuhamasisha idadi kubwa ya
wananchi kujiunga na mfumo wa kulipia kabla gharama za matibabu ili
kuzuia vifo visivyo vya lazima katika jamii.
Bendera alisema ili kuiwezesha serikali kufikia lengo lake la
kufikisha huduma bora za afya kwa kila mtanzania kuna umuhimu wa
kipekee kwa halmashauri zinazounda mkoa huo kuhakikisha wananchi wote
wanajisajili katika iCHF wakiwemo maskini ili nao waweze kuhakikishiwa
upatikanaji wa matibabu.
“Kwa kutambua changamoto ya kutokuwepo rasilimali za kutosha katika
vituo vya kutolea huduma ndio maana serikali iliamua kuanzisha mfumo
huu wa kuchangia kidogo kila mwaka gharama za matibabu kabla ili
kumwezesha kila mwananchi kupata matibabu kwa nia ya kuchangia fedha
kidogo.”, alisema.
Aidha aliongeza, “Wito wangu kwenu wananchi ni jiandikisheni kwa wingi
kwasababu ugonjwa haupigi hodi… kwa upande wa halmashauri hebu anzeni
kuweka fedha kwa mpango mtakaokubaliana ili wale maskini nao waweze
kusaidiwa kupata matibabu kama wenzao wengine wenye uwezo wa
kuchangia”, alisema.
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) Eugine Mikongoti akizungumza katika uzinduzi huo aliwataka
watoa huduma za afya kupitia iCHF kumaliza malalamiko ya wagonjwa kwa
kuhakikisha michango yote ya wananchi inatumika ipasavyo kwa ajili ya
kununulia dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha kuona thamani halisi ya
fedha zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa PIA alisema katika miezi sita
kuanza kwa utekelezaji wa iCHF humo idadi ya wananchi wanaojiunga
inaongezeka kwa kasi kutokana na kuongezwa kwa idadi ya vituo vya
kutolea huduma, maduka ya dawa, ushirikihswaji jamii na uhamasishsaji

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »