Mjumbe wa Kamati ya utendaji
ya TFF na makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Said Mohamed leo
amefungua kozi ya makocha wa golikipa inayoendelea katika ofisi za TFF zilizopo
Karume.
Katika ufunguzi wa kozi
hiyo, Said amesema anashukuru FIFA kwa kuwapa nafasi ya kuendesha mafunzo hayo
ya makocha wa makipa kwa mara ya kwanza nchini, na kuwaomba washiriki wa kozi
hiyo kutumia nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Jumla ya makocha 31
wanashiriki kozi hiyo kutoka vilabu vyote viliyovopo Ligi Kuu na magolikipa wa
zamani waliodakika timu za Taifa.
Kozi hiyo ya makocha wa
makipa inaendeshwa na mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka nchini Ufaransa, ambapo
kozi hiyo itafungwa rasmi tarehe 17 Julai mwaka huu.
EmoticonEmoticon