NA MWANDISHI WETU
Mwandishi wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore ametangaza kugombe
Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro,
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada
ya kujipima na kutafakari juu ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same
Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo
yaliyokwama kwa miaka mingi.
Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo
yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa
Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini,
anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia
kwa uhakika.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa
kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa
wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana
na matatizo waliyonayo.
“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya,
Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi
hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua
kwa haraka na wakati unaofaa,” alisema Kakore.
Kakore ni mwandishi mkongwe wa
habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo
alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya
Tanzania.
Jimbo la Same Magharibi kwa sasa
linashikiliwa na David Mathayo David ambaye amekaa kwenye kiti hicho kwa
miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa. Mionggoni mwa watu wa kwanza kuwa
wabunge kwenye Jimbo hilo ni aliyewahi kuwa waziri katika katika
serikali ya awali ya kwanza, Marehemu Chediel Mgonja.
EmoticonEmoticon