Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Kushoto akimkabidhi Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi Mwenge wa Uhuru baada ya kumaliza ziara
yake Mkoani Rukwa na kuanza ziara zake Mkoani Katavi tarehe 15 Julai
2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (wa nne kulia mbele) na wakimbiza
mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya
kuukabidhi Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2015 baada ya kumaliza ziara
yake Mkoani Rukwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (wa kwanza mbele) na wakimbiza
Mwenge kitaifa na kimkoa wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani
Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji
katika Kijiji cha Kalundi Wilayani humo tarehe 14 Julai 2015.
Moja
ya mtambo wa kisasa wa umwagiliaji katika shamba la umwagiliaji la
Ntatumbila Wilayani Nkasi. Mradi huu wa shamba la umwagiliaji na mifugo
lina ukubwa wa hekta 1,000 na linamilikiwa na kuendeshwa na wazawa
ambapo mpaka kukamilika kwake utagharimu fedha za kitanzania shilingi
bilioni 46.
Miongoni
mwa wamiliki wa shamba hilo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
kitaifa ndugu Juma Khamis Chum wakipiga picha ya pamoja na Mwenge wa
Uhuru mara baada ya uzinduzi wa mradi wa umwagiliaji katika shamba hilo
la Ntatumbila Wilayani Nkasi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
EmoticonEmoticon