BOSS WA UN, ALVARO RODRIGUEZ ATEMBELEA SABASABA, ASEMA MAONYESHO NI FURSA YA KUJIFUNZA

July 02, 2015
IMG_5941
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_5945
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati wakielekea katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lilipo Karume Hall mara tu baada ya kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi na mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa dunia sasa imekuwa kijiji kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo unakusudia kuendelea kuwepo kushirikiana na watanzania katika kutatua matatizo kwenye Nyanja mbalimbali.
Bw. Alvaro amewataka watanzania kusherehekea pamoja miaka 78 ya Umoja hapa nchini kwa kutoa maoni mbali mbali na kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo.
Amesema kwa pamoja tunahitaji kuzungumzia usawa wa kijinsia, masuala ya kisiasa, mabadiliko ya tabia nchi na mambo ya kiuchumi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa kufanya juhudi za kusaidia vijana kuanzia ngazi za chini kabisa na kuwawezesha kuwa wajasiriamali.
Amesema kitendo cha Umoja huo kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba sambamba na kijana Amos Mtambala waliyemuwezesha kwa kumpatia mafunzo ya sanaa za uchoraji kumeleta hamasa kubwa miongoni mwa vijana wasio na ajira nchini.
IMG_6027
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_6032
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5959
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu, akitoa maelezo jinsi wanavyoelimisha wananchi kuhusiana shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini sambamba na malengo ya millenia yanayofikia kileleni kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko walipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5962
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akielezea maeneo ya Program mbalimbali za UNDAP yaliyofanikiwa nchini Tanzania kwa Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) aliyeambata na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko.
IMG_5965
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akikabidhi taarifa ya mwaka ya UNDAP kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (katikati) aliyefuatana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) walipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall.
IMG_5973
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akitoa maelezo jinsi alivyowezeshwa kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5981
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini, Magnus Minja akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuhusiana na program ya kazi njenje ya mradi wa kufundisha vijana katika shughuli za ujasiriamali inayoratibiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambapo kijana Amos iliweze kumuinua na kujiajiri kupitia sanaa ya uchoraji.
IMG_5995
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko, akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya karatasi inayotoa maelezo ya jinsi ya Watanzania wanavyoweza kushiriki kutoa maoni mbalimbali juu ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kutuma SMS ambayo ni bure bila malipo yoyote na moja kwa moja kumfikia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Ambapo pia njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kubofya link hii http://gpl.cc/UN2
IMG_6021
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na waaandishi wa habari katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa ambao wanashiriki maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_6038
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko mfuko wenye machapisho na vijarida mbalimbali vya Umoja wa Mataifa.
IMG_6467
Afisa Utawala wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Magoma (wa pili kushoto) akiuliza swali kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama na Wa pili kulia ni Mchumi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vainess Molle.
IMG_6476
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez akijibu swali la Bw. Suleiman.
IMG_6494
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akionyesha namna ya kutoa maoni ya utendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya SMS ambayo ni bure kwa mitandao yote ya simu za mkononi nchini kwa wadau waliotembela banda la UN Tanzania.
IMG_6435
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez ajibu maswali mbalimbali yalitumwa kwa njia ya mtandao na wananchi katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_5997
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini, Alvaro Rodriguez na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma katika banda la Umoja wa Mataifa maonyesho ya Sabasaba.
IMG_6456
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja na Mkuu wa UN Tanzania.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »