Mstahiki
Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi
mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.
Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .
Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.
Lengo la
mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya
awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya
miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.
Katika
kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi
(Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na familia ya
walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha
bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na
kuwaua wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania
EmoticonEmoticon