Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini |
Na Mwandishi Wetu
Mbunge
wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Januari
Makamba a ushanmewaomba wanachama wenzake wa CCM walioko Njombe
kutochukulia suala la ugombea kwa ushabiki kiasi cha kuzua mtafaruku
ndani ya chama, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wake.
Makamba
ameyasema hayo alipokuwa akiwashukuru wanachama wenzake waliojitokeza
kumdhamini ili kupata ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi
Oktoba mwaka huu.
"Najua
katika kipindi hiki, ambacho wanachama wengi tumejitokeza kuwania
nafasi hii kila mtu ametengeneza kundi la wafuasi ambao wengi wanadhani
kwamba kuwa kundi la mtu mmoja basi wewe ni adui wa kundi jingine. Hili
ni kosa, sote tunania njema na nchi hii, tujenge mazxingira ya
kutooneana haya baada ya kupatikana kwa mgombea mmoja kwa kuungana mkono
bila kuchafua wengine", alisisitiza Makamba.
Makamba
ameonya pia kuhusu kuchafuana kwa watangaza nia, wenyewe kwa wenyewe
ambako kutasababisha kazi nyingine kubwa ya kuanza kumsafisha mgombea
atakayesimamishwa na chama muda utakapofika.
Leo mchana Makamba anatarajiwa kupokea wadhamini mkoani Songea na baadae kuelekea Mbeya mjini ambako pia atafanya zoezi hilo.
Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini
Mh
January Makamba na mkewe wakiwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Njombe
ambapo walipokelewa na wanachama wa CCM aliokuwa na kikundi cha ngoma
Mh January Makamba na mkewe wakisalimana na baadhi ya wanachama wa CCM katika ukumbi mdogo wa CCM mkoani Njombe.
Mh January Makamba akiwaka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM mkoa wa Njombe.
Mh
January Makamba akipokea fomu yenye majina ya wanachama wa CCM wa
Njombe waliomdhamini kutoka kwa katibu wa CCM moa wa Njombe, ndugu
Mponzi. idadi ya wanachama waliojitokeza kuweka sahihi ya kumdhamini ni
72.
Mh
January Makamba akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika
Ukumbi mdogo wa CCM mkoa wa njombe. January amepata idadi ya sahihi 72
za wanachama waliojitokeza kumdhani kumwezesha kupitishwa na kupewa
ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu
wa CCM mkoa wa Njombe akizungumza na wanaCCM wa Njombe kabla ya
kumkaribisha Mh January Makamba kuzungumza na wanachama wa CCM wa
Njombe. ambapo amepata idadi ya sahihi 72 za wanachama waliojitokeza
kumdhani kumwezesha kupitishwa na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mh
January Makamba akimsikiliza kwa makini katibu wa CCM mkoa wa Njombe,
ngugu Mponzi walipofanya mazungumzo mafupi ofisini kwa katibu huyo. mara
baada ya kupokea fomu zenye sahihi za wanachama wa CCM waliomdhamini.
January amepata idadi ya sahihi 72 za wanachama waliojitokeza kumdhani
kumwezesha kupitishwa na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.