Raisi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi, Pierre
Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini Tanzania saa moja baada ya
kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi mkuu wa majeshi yake
Meja jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba amempindua.
Jenerali huyo mara baada
ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa kiwanja cha kimataifa cha
ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata hivyo haiko wazi
ikiwa jeshi linamuunga mkono Meja jenerali Godefroid Niyombare. Naye
msemaji wa rais wa Burundi, amesema kwamba wanajeshi watiifu kwa Rais
ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa viongozi nchini Tanzania, amesema
nchi iko shwari.
Maelfu ya watu wamekuwa
katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo Bujumbura baada ya
wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya kugombea
muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu wa kanda
wamelaani mapinduzi hayo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu elfu tatu
walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na watutsi ,vita
vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini humo umehusisha
kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa. lakini,yaliyojiri Burundi
hayana tofauti na kilichojiri katika nchi jirani ya Rwanda ambayo
ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa na masuala ya ukabila.
Umoja wa mataifa umeonya
hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani
na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea katika vita vya
wenyewe kwa wenyewe .
CREDIT: BBC
EmoticonEmoticon