Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu ambaye
alikuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu utendaji wa Shirika hilo leo
asubuhi. Waziri Lukuvi yuko katika ziara ya siku mbili kushuhudia
utendaji wa Shirika hilo ambapo leo na kesho atatembelea baadhi ya
miradi ya NHC iliyopo jijini Dar es Salaam na kisha baadaye kuzungumza
na wafanyakazi wa NHC.
Picha za Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na James
Rhombo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NHC, wakati akikaribishwa Makao
Makuu ya NHC. Kulia na Felix Maagi, Hamad Abdallah na Raymondo
Mndolwa.
Waziri Lukuvi akisindikizwa na
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa,
Haikamen Mlekio kuingia kwenye ofisi za makao makuu ya NHC leo.
Waziri Lukuvi akisalimiana na
Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, wakati akikaribishwa Makao
Makuu ya NHC. Kulia kwa Maagi ni James Rhombo, Hamad Abdallah na
Raymondo Mndolwa.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa
na Utawala wa Shirika la NYumba la Taifa Raymond Mndolwa, akimsindikiza
Waziri Lukuvi kuingia ukumbini NHC ambapo alipata fursa ya kuwasalimia
wafanyakazi wa shirika hilo.
Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC
Waziri Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa NHC
Wakurugenzi wa NHC
Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)
Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza Waziri Lukuvi (hayupo pichan)
Waziri Lukuvi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NHC katika picha.
EmoticonEmoticon