NA MWANDISHI WETU,KOROGWE.
JESHI
la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia mkazi mmoja wa Kwa mathias Kibaha Mkoani
Pwani kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu wapatao
13 raia wa Ethiopia jambo ambalo ni kosa kisheria
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga, Fresser Kashai aliwaambia waandishi wa habari kuwa
tukio hilo lilitokea Januari 2 mwaka huu saa kumi na mbili na nusu jioni kwenye
kijiji cha Semkiwa wilayani Korogwe ambapo walikamatwa watuhumiwa hao.
Alimtaja
mtuhumiwa huyo kuwa ni Magomba Daudi (42) mkazi wa Kwamathias Kibaha Mkoani
Pwani ambaye alikamatwa na Jeshi hilo akiwa amewahifadhi wahamiaji haramu hao kwenye
gari lenye za usajili T.218 DLC Toyota Noah linalomilikiwa na Mohamed Kibwanga.
Kamanda
Kashai alisema kuwa dereva huyo alikamatwa akiwa anawasafirisha wahamiaji
haramu hao ambao ni raia wa Ethiopia wakati akijua kufanya hivyo ni kuvunja
sheria za nchini.
Aliwataja
wahamiaji haramu waliokamatwa ambao ni raia wa ethiopia kuwa ni Mackimu
Daniel(20),Balachu Tamire(21),Elias Yacon(22),Anado Dafacho(24),Lambare
Tamire(20),Gefachew Mohamed(22),Tadesse Hebebo(23).
Aidha
aliwataja wengine wanaoshikiliwa ni pamoja na Wolde Baremo(23),Tistu
Aubab(23),Testye Bekd (26),Vusto Pexros (25),Hatmu Lalgu (23) ambapo watuhumiwa
wote hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili baada ya
upelelezi wa awali kukamilika.
Hata
hivyo,Kamanda Kashai alitoa wito kwa wananchi kuacha kujishughulisha na
biashara za uhamiaji haramu kwa sababu kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria na
huenda wakaishia mikononi mwa Polisi badala yake wafanye biashara nyengine
ambazo zinaweza kuwaingizia kipato halali.
“Mimi nadhani ufike wakati ambao wananchi na
jamii kwa ujumla itambue kuwa biashara wa wahamiaji haramu ina madhara makubwa
hivyo hatuna budi kuachana nayo na kuangalia kazi mbadala zitakazoweza
kuwaingizia kipato “Alisema Kamanda Kashai.
|
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon