BUNGE MAALUM LAPITISHA AZIMIO LA KURA YA MSETO
Na Magreth Kinabo – MAELEZO, Dodoma
Hatimaye
baada ya mvutano wa baadhi wa wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba
kuhusu upigaji wa kura ya siri na ya wazi kuendelea leo Mwenyekiti wa
Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Pandu Ameir Kificho
amewasilisha azimio la mapendekezo ya ya upigaji kura wa wazi na
siri kutumika kwa pamoja katika kaununi ya 37 na 38, ambalo
limetipitishwa na Bunge hilo kwa matokeo ya jumla kwa kura ya ndiyo
376 na hapana 133 .
Kura
hizo zimetangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge ,hilo,
Mhe.Samia Sululu kabla ya kuahirisha kikao hicho leo usiku,
ambapo alisema azimio hilo limepitishwa na Bunge hilo ,
kufuatia upigaji wa kura ,ambapo idadi ya kura zilizopigwa ni 509,
wakati mauhudhurio ya wajumbe yalikuwa 511.
Mhe
. Samia alisema kwa upande wa kura za wazi zilizopigwa ni 438, ambazo
za ndiyo zilikuwa 351 na hapana ni 87, wakati kura za siri zilizopigwa
zilikuwa ni 71, ambazo za ndiyo zilikuwa 25 na hapana ni 46.
Uamuzi
huo umefuatiwa baada ya hali hiyo ambayo ilitokea tena kwa mara
nyingine jana jioni mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na
Haki za Bunge Maalum, Mhe . Kificho kuwasilisha mapendekezo ya upigaji
kura wa wazi na siri kutumika kwa pamoja katika kaununi hizo.
Tangu
jana jioni na leo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakitoa michango kutaka
upigaji kura huo uwe wa wazi na siri , huku wengine kutaka kura ya
siri.
Awali Kanuni
za 37 na 38 zilibaki kiporo tangu wakati wa utungaji wa
kanuni mbalimbali za Bunge hilo, na uchangiaji wa kuziboresha,
kutokana na mvutano huo, ambao baadhi ya wajumbe kutaka kura ya uwazi
na wengine siri.
Wakizungumzia
juu ya makubaliano yaliyofanywa na Kamati ndogo ya Muda ya
Maridhiano na Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge kuhusu mapendekezo ya
upigaji kura huo.
Mmoja
ya wajumbe wa Kamati hiyo ndogo ya Maridhiano, John Nyika
alisema walifanya mazungumzo hayo waliona ni vema wakubaliana mtu
anayeweza kupiga kura ya uwazi na anayetaka ya siri wapige kulingana na
matakwa yao ili kuwezesha mchakato huo kupiga hatua mbele.
“
Tunaomba utaratibu huu wa maridhiano uendelee … ili tuweze
kupiga hatua mbele,” huku akisisitiza hawana dhamira yoyote
ya kukwamisha mchakato wa Katiba mpya. Hivyo watakuwa wa kwanza kuunga
mkono kwa kura azimio litakalopitishwa kwa kura zitakazokubaliwa.
Naye
mjumbe mwingine wa kamati hiyo , Vuai Ali Vuai alisema jambo hilo ni
kubwa kwa Watanzania ndio maana wanatakiwa kupiga kura kwa uwazi umma
uweze kuona .
Kwa
upande wake ,mjumbe mwingine wa kamati hiyo ya ndogo ya Maridhiano
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela
amesema ni vizuri wajumbe hao wakakubali azimio hilo kwa kuwa mpaka
sasa wameshatumia siku 40 kujadili kanuni za kuongoza Bunge hilo na
zimetumia gharama hivyo wasiendelee kuongeza gharama, zipo siku tatu za
kuomba ili kufanikisha maridhiano hayo.
“
Ninawaomba wajumbe wenzangu kukubali azimio hili ili tuweze kusonga
mbele na na mchakato wa kupata Katiba ,” alisema Askofu Mtetemela.
EmoticonEmoticon