Na Oscar
Assenga, Tanga.
TIMU za soka
Mgambo Shooting na Coastal Union zote za mkoani Tanga leo zimeshindwa
kutambiana baada ya kulazimisha suluhu pacha ya kutokufungana katika mchezo wa
ligi kuu Tanzania
bara uliochezwa dimba la soka Mkwakwani.
Katika mchezo
ambao ulikuwa wa kawaida ulishuhudiwa mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza
timu hizo zikitoka sare ya kutokufungana mchezo ambao ulikuwa mkali.
Raundi ya lala
salama katika mchezo huo ilianza kwa kasi ambapo kila timu iliweza kulisakama
lango la mwenzie kwa kushambuliana kwa zamu ambapo kwenye dakika ya 60 Mgambo
Shooting walifanya mabadiliko kwa kumtoa Martin Mlolera na kumuingiza Full
Maganga huku Coastal Union wakimuingiza Yayo Lutimbba na kumtoa Seleman Kassim
Selembe.
Hali kadhalika
Coastal Union kwenye dakika ya 71 walimtoa Haruna Moshi Boban na kumuingiza
Daniel Lyanga ambapo kutokana na mabadiliko hayo,Coastal Union waliweza
kuimarisha nguvu ambapo dakika 72 Yayo Lutimba alimanusura aipatia bao timu
hiyo baada ya kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi uwanjani.
Kikosi cha
Coastal Union leo kiliwakilishwa na mlinda mlango,Shabani Kado,Hamad
Hamisi,Othumani Tamimu,Mbwana hamisi,Juma Nyoso,Jerry Santo,Uhuru Seleman,Crispine
Odulla,Daniel Lyanga,Keneth Masumbuko.
Kwa upande wa
Mgambo Shooting,Mlinda Mlango,Godson Mmasa,Salum Mlima Bashiru Chanache,Novart
Lufunga,Bakari Mtama,Salum Kipanga,Malimi Busungu,Mohamed Samata,Omary
Juma,Martin Mlolera na Peter Mwalyanzi.
EmoticonEmoticon