NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imesema uwakilishi wa ujumbe kwenye Mkutano Mkuu unaanzia
kwenye chama cha mpira wa miguu cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na
baadaye klabu ya Ligi Kuu.
Mwongozo
huo juu ya uwakilishi wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu umetolewa kutokana
na maombi ya Sekretarieti ya TFF kwa kamati hiyo iliyokutana jana
(Septemba 16 mwaka huu) baada ya kubaini baadhi ya wajumbe wanashikilia
nafasi mbili kwenye vyama tofauti.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba, kuna makundi ya aina tatu ya wanachama
wanaounda TFF. Makundi hayo ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu
za Ligi Kuu.
Sekretarieti
ya TFF imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kuchaguliwa wa mikoa
ambao pia ni viongozi wa vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu, hivyo wana
nafasi zaidi ya moja ya kuingia kwenye Mkutano Mkuu.
Hivyo,
kutokana na mwongozo huo ushiriki wa wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa TFF
utaanzia chama cha mkoa, kufuatiwa na chama shiriki na baadaye klabu za
Ligi Kuu.
Pia
nafasi ambazo zinaweza kuwakilishwa kwenye Mkutano Mkuu kama mhusika
hayupo ni za Mwenyekiti atakayewakilishwa na Makamu Mwenyekiti, na
Katibu atakayewakilishwa na Katibu Msaidizi. Nafasi za ujumbe wa Mkutano Mkuu na ile ya mwakilishi wa klabu hazina uwakilishi kama mhusika hayupo.
EmoticonEmoticon