Na Selemani Kibugo,Muheza
SERIKALI wilayani Muheza imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha wanajenga vituo vya Afya kila kata wilayani humo ili kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi wake
Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Muheza, Herbert Mntangi wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mashewa,Kilongo,Tingeni na Kisiwani Kata ya Kisiwani.
Amesema kuwa serikali inampango wa kujenga vituo vya Afya kata zote pamoja na Zahanati ambapo hiyo ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM natayari vituo vitatu vimeshaanza kujengwa ambako ni Songa,Ubwari naMisalai ambavyo ni vya kisasa.
Kwa upande wa elimu amesema kuwa wanakusudia kuipandisisha hadhi shule ya sekondari Shebomeza kuwa ya kidato cha tano na sita na watajenga kila Tarafa sekondari moja ya kidato cha tano na sita na kuahidi walimu wamsingi na sekondari kuboreshewa huduma za nyumba na maslahi.
EmoticonEmoticon