Na Oscar Assenga, Mkinga.
MKUU wa wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza amewataka
vijana kupenda michezo na kuithamini kwa kuwa michezo ni ajira ambayo inaweza
kuwainua kimaisha endapo wataizingatia na kucheza kwa umakini.
Mgaza alitoa wito huo jana wakati akifungua
Mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi wilayani humo (Umitashumta) ambapo
alisema michezo pia huongeza upendo ushirikiano baina ya wachezaji wanaokuwa
wakishiriki ikiwemo kujenga undugu miongoni mwao.
Amesema michezo pia inadumisha amani kwa kuwa
watu wanaposhiriki katika michezo wanakuwa ndugu na kufikiria jinsi ya kupata
mafanikio hivyo kupelekea kudumisha amani tulionayo.
Aidha amewataka washiriki kucheza vizuri ili
kuweza kutengeneza timu nzuri ya wilaya ambayo itaanza kambi kwa ajili ya
kuwakilisha wilaya hiyo katika mashindano hayo ngazi ya mkoa.
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mashindano hayo, Afisa Elimu wilaya ya Mkinga Idara ya Elimu Msingi, Juma Mhina
amesema mashindano hayo yanashirikisha timu kutoka tarafa mbili ambazo ni
Mkinga na Maramba na inashirikisha idadi ya wanamichezo 190.
Mhina amesema michezo itakayochezwa ni
Pete,Wavu, Mpira wa Miguu na Mpira wa mikono na kueleza kuwa lengo la serikali
kurudisha michezo mashuleni ni kuibua vipaji vya wachezaji kuanzia mashuleni.
Mwisho.
EmoticonEmoticon