MCHEZAJI
nyota maarufu wa tenisi kutoka Uingereza Andy Murray amejitoa katika
michuano ya wazi ya Ufaransa kutokana na maumivu ya mgongo yaliyopelekea
kushindwa kuendelea kucheza katika michuano ya wazi ya Italia. Murray
ambaye anashika namba mbili katika orodha za ubora Duniani kwa upande
wa wanaume amejitoa katika michuano hiyo baada ya kushauriwa na
madaktari wake na anatarajia kurejea tena uwanjani katika michuano ya
Wimbledon katikati ya mwezi ujao. Nyota
huyo ambaye ni bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani amesema umekuwa
ni uamuzi mgumu kufanya kwani huwa anapenda kucheza jijini Paris lakini
imekuwa nje ya uwezo wake kwasababu ya ushauri wa kiafya aliopewa. Murray
aliwaomba radhi waandaaji wa michuano hiyo na kuwashukuru mashabiki
wake kwa kumtumia ujumbe wa kumuunga mkono na sasa kazi kubwa aliyokuwa
nayo ni kuhakikisha anapona na kurejea haraka uwanjani.
EmoticonEmoticon