Na Oscar Assenga, Tanga.
IMEELEZWA kuwa mradi wa
kituo cha kupozea umeme kilichopo Sahare (33/11Kv,15MVA)ni muendeleo wa Juhudi
za serikali kuu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini kuendeleza
usambazaji wa umeme wa uhakika katika maeneo yote hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkurugenzi wa Millenium Challenge Tanzania,Mhandisi,Ipack Chanji wakati
akitoa taarifa ya mradi wa kituo hicho kidogo cha kusambazia umeme Sahare kwa
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2013 ambapo amesema mradi huo
ulianza Juanri mwaka 2011 na unatarajiwa kukamilika Julai 2013.
Chanji amesema mradi huo
ni utatumia kiasi cha (dola 1,541,408.95) ambazo ni sawa na shilingi za
kitanzania 2,508,643,066.12(Bilioni mbili milioni mia tano na nane,laki sita
arobaini na tatu elfu sitini na sita na senti kumi na mbili) zilizopatikana
kupitia akaunti ya changamoto za millennia ikiwa ni msaad wa watu wa marekani.
Amesema faida za mradi
huo ni kuongeza nguvu ya umeme hasa kwa maeneo ya viwandani kitendo ambacho
kitavutia wawekezaji ndani na nje pamoja na kupatikana umeme wa uhakika kwa mahitaji ya nyumbani na
maofisini na hivyo kuongeza tija kwenye uzalishaji mali hasa za viwandani
ikiwemo kukua kwa pato la Taifa.
Mwenge huo umezindua miradi 7 yenye thamani ya
bilioni 8 katika wilaya ya Tanga ambayo ni maabara katika shule ya sekondari
st.christina,barabara ya viwandani,chama cha ushirika wafugaji maziwa
kichangani,umeme,
Mwisho.
EmoticonEmoticon